loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Guardiola: Ninastahili mkataba mpya

KOCHA Pep Guardiola amesema anastahili kuongezewa mkataba Manchester City badala ya kupewa tu.

Mkataba wa sasa wa Mhispania huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu na uongozi wa City unamtaka abaki.

Guardiola, mwenye umri wa miaka 49, anaanza msimu wake wa tano, City kucheza na Wolves leo, ukiwa ni muda mrefu zaidi ya miaka aliyodumu Barcelona na Bayern Munich.

"Ningependa kukaa hapa kwa muda mrefu," alisema."Ni mahali ninapenda kuwa lakini lazima nistahili. Klabu hii ilifikia viwango katika muongo mmoja uliopita lakini lazima tuendelee kudumisha hiyo."

Guardiola alisema Mwenyekiti, Khaldoon Al Mubarak na Mtendaji Mkuu, Ferran Soriano hawajazungumza naye juu ya hali hiyo.

Walakini, baada ya kukatishwa tamaa kwa msimu uliopita, walipomaliza kwa alama 18 nyuma ya mabingwa Liverpool na kutolewa kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa bila kutarajiwa na Lyon, ambao wakati huo walipigwa kirahisi na Bayern Munich katika nusu fainali, kuna shinikizo kwa Guardiola kuboresha matokeo.

"Hawakuniambia lazima ufanye hivi au vile, waliniambia nicheze," alisema Guardiola"Lakini najua viwango vya klabu na ikiwa sitafikia viwango, labda sistahili kwa hivyo lazima nishinde kuongeza mkataba wangu."

 

TIMU za Liverpool na Chelsea jana zilibanwa mbavu baada ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi