loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake watakiwa kuchangamkia fursa katika soka

MKUFUNZI wa kimataifa, Henry Tandau amewahimiza wanawake waliohitimu mafunzo ya Uongozi na Utawala katika mpira wa miguu kuchangamkia fursa zitakazojitokeza katika soka.

Tandau aliyasema hayo Dar es Salaam juzi, wakati akifunga mafunzo hayo ambayo yalihudhuriwa na wanawake 38, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ikiwa ni mpango endelevu wa kuwawezesha kushiriki katika uongozi nchi nzima.

Alisema anatamani kuona kati ya wahitimu hao, baadhi yao waje kuwa viongozi wakubwa akitolea mfano rais na nafasi nyingine za juu huku akijivunia kuna baadhi ya viongozi walioko TFF aliwahi kuwafundisha na leo ni watu wakubwa katika uongozi.

“Ni matumaini yangu baadaye nitaona kati ya ninyi wapo watakaokuwa viongozi wakubwa. Lengo ni kuona ninyi mnagombea nafasi mbalimbali, mnaweza kuwa viongozi kwenye klabu, vyama vya michezo na mashirikisho,” alisema.

Alisema mafunzo hayo yameanza Dar es Salaam ila yataendelea katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza, Geita, Mbeya, Songea na Zanzibar.

Kwa upande wake, mdhamini wa mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki ya KCB, Christine Manyenye ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wanawake kutoona mafunzo hayo kama ni jambo dogo bali wachukue kwa ukubwa na kusonga mbele.

Alisema uongozi wa mwanamke unatakiwa kuanzia ngazi ya familia na wanachotakiwa kufanya ni kujitambua, kujiamini na kutafuta  fursa watakazoziona.

“Kinachotuangusha wanawake wengi hatujiamini katika uongozi, mnatakiwa mbadilike kama ni changamoto huwa zipo na ndizo zinazotusaidia kutuweka imara,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wahitimu ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM, Tunu Shenkome alishukuru TFF kwa kuwapa nafasi ya mafunzo hayo na kuahidi kile walichokipata watakwenda kukitumia.

“Tutakwenda kutumia kwa vitendo kile tulichokipata, naimani  TFF wataendelea kutoa kozi hii kwa wengine ili kuwapata wanawake wengi katika uongozi wa soka,” alisema.

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza Septemba 15 na kumalizika juzi.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi