loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yondani asajiliwa Namungo

BEKI  wa zamani wa Yanga, Kelvin Yondani  amesajiliwa  na Namungo FC kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.

Yondani aliyeitumikia Yanga kwa misimu nane mfululizo tangu alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea Simba, aligoma kuongeza mkataba  wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa sababu za kimaslahi.

Akizungumza kutoka mkoani Lindi ,Katibu Mkuu wa Namungo, Ally  Selemani  alisema usajili wa beki huyo mkongwe ni kwa ajili  ya kuimarisha kikosi chao hasa sehemu ya kiungo kujipanga na mechi za ligi na ile ya Kombe la Shirikisho Afrika.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi