loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hazina yataka Shirika la Posta wapunguze matumizi

MSAJILI wa Hazina, Athumani Mbuttuka ameitaka bodi ya Shirika la Posta Tanzania kupunguza matumizi na pia upimaji kazi kwa memenja wa mikoa, uwe kwa kufikiwa viwango cha ukusanyaji mapato kwa faida.

Mbuttuka aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo kwa viongozi wa shirika hilo.

Alisema pamoja na shirika hilo kuwa na mabadiliko makubwa na kutoa gawio serikalini, bado gharama za uendeshaji ziko juu.

"Tumeweka vigezo vya gharama za uendeshaji ambapo zinatakiwa zisizidi asilimia 50, lakini bado shirika linajiendesha kwa gharama ya asilimia 75, hivyo bodi inapaswa kuangalia matumizi ya shirika."alisema Mbuttuka.

Alisema ni vyema kila tawi la shirika hili, lihakikishe linapata faida na washindane kwa kadri faida inavyotengenezwa ili kuongeza gawio kwa serikali.

"Muweke malengo ya kukusanya faida, mfano mtu yupo tawi la katikati ya mji, kwa mwaka awekewe zikusanywe faida ya shilingi milioni 350 kwa kuja na ubunifu mbalimbali, hivyo kama hujafikisha utapaswa kupisha ili aingie mwingine."alisema Mbuttuka na kuongeza;

"Kwa miaka mitatu mfululizo mmejitahidi kutoa gawio, miaka miwili mmetoa shilingi milioni 350 kila mwaka, ule mwaka mwingine mmetoa shilingi milioni 250, mnajua haitoshi kwa ukubwa wa shirika hili, haiwezekani, tunatarajia kwa muda mfupi ujao tuanze kuzungumzia bilioni na najua hili linawezekana" alisema.

Aidha, Mbuttuka alisema ofisi yake inakamilisha mikataba, ambayo itakuwa na malengo ya kupima shirika hilo.

"Tunataka tukikupima tukupime kwa kitu sahihi, katika muda mfupi ujao mtapata na kusaini mikataba mipya ili kuhakikisha kwamba Shirika la Posta linakuwa na tija kulingana na vigezo vya kupima ufanisi."alisema.

Mbuttuka alilipongeza shirika hilo kutoka kwenye faida hasi na kuwa na faida chanya.

"Kila biashara mnayoifanya mhakikishe inajiendesha kwa faida, ili tuondokane na biashara moja kujiendesha kwa faida, nyingine kwa hasara hivyo kubebwa na ile inayofanya vizuri."alisema.

Kuhusu biashara ya usafirishaji wa sampuli za damu, Mbuttuka alisema shirika limeaminiwa na serikali kupewa jukumu hilo kwa ustawi wa nchi na kuwataka kuwa makini ili serikali kuendelea na imani na shirika hilo.

Alikemea migogoro sehemu ya kazi, kwa kuwa imekuwa ikirudisha nyuma utendaji wa shirika.

Posta Masta Mkuu Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe, alisema shirika hilo liliweka utaratibu wa kutoa mafunzo kwa viongozi wa juu ili kuongeza ufanisi katika utendaji.

Alisema mafunzo hayo yameweka mwelekeo mmoja wa utendaji kazi, ambapo kuna viwango vya ufanisi vimewekwa, ambapo kila Meneja wa Mkoa anatakiwa awe amezalisha asilimia 75 ya bajeti Shirika.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi