loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi wafurika Tawa kuomba kufuga wanyamapori

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) imepokea maombi ya kutosha ya watu binafsi ya wanaohitaji kuanzisha ufugaji wa wanyamaapori kwenye mashamba, ranchi na bustani hapa nchini.

Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Tawa, Mabula Nyanda alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro kuhusu mikakati mbalimbali inayochukuliwa na mamkala hiyo kwenye suala la usimamizi wa wanyamapori nchini.

“Ni kweli tulitangaza watu wenye nia ya ufugaji wa wanyamapori kwenye mashamba, ranchi na bustani na tumepokea maombi ya kutosha, tumeshaanza akutoa vibali kwa wananchi na mwitikio ni mkubwa wa kuanzisha hayo mashamba ya ufugaji wanyamapori ” alisema Nyanda.

Pamoja na mwitikio huo mkubwa, Nyanda alitaja changamoto inayowakabili watu waliowasilisha maombi yao ni kuwepo kwa gharama kubwa kutoka kwa watu binafsi ama kampuni zenye kuhusika na ukamataji wa wanyamapori.

Katika hatua nyingine, Tawa imeshalifanyia kazi agizo la Rais John Magufuli la kuanzishwa kwa mabucha ya nyamapori hapa nchini.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake kuangalia utaratibu wa kufanya biashara hiyo hapa nchini.

Hivyo Kaimu Kamishna wa  Uhifadhi wa Tawa, alisema mara baada ya kupokea agizo hilo, walifanyia kazi kwa kufanya tathimini ya kitaalaamu na kuangalia mabucha ya ania hiyo yatafunguliwa maeneo gani na watu watakaohusika kuyaendesha .

Alisema tathimini hiyo iliangalia nyama hiyo itakayouzwa  itatoka wapi , uthibiti wa hiyo nyamapori utafanywa utatoka wapi kwa vile inahitajika taasisi nyingine za serikali kama Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi ili kuthibitisha usalama wake kwa mlaji .

Pia alitaja eneo jingine lililofanyiwa tathimini ya kitaalamu ni namna ya kujiandaa kama Tawa katika usimamizi kwa kusababu ya kudhibiti kuibuka tena kwa ujangili.

“Kwa hiyo tayari tumekamilisha tathmini yetu na utakuwepo mwongozo, huwenda wiki hii au wiki ijayo Wizara ya Maliasili na Utalii itatamka rasmi juu ya masuala ya mabucha ya nyamapori,” alisema Nyanda.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi