loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Profesa Lipumba aahidi Muungano wa kiuchumi

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania anakusudia kuleta mabadiliko makubwa ya Muungano kutoka wa kisiasa na kuwa wa kiuchumi zaidi, ili kuwanufaisha wananchi.

Mgombea huyo alisema hayo katika mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba  jana, ambapo pia alimtambulisha mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Mussa Haji Kombo.

“Muungano ni tunu ya kitaifa ambayo inatakiwa kuenziwa kwa nguvu zote, kwani umesaidia kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara na kuishi wakiwa ndugu.”

“Nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitahakikisha Muungano unakuwa imara, huku ukijikita zaidi kuwanufaisha wananchi kiuchumi katika masuala ya biashara,'' alisema.

Awali, mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CUF, Kombo alisema akichaguliwa kuwa Rais wa visiwa hivyo, anakusudia kuimarisha sekta ya elimu pamoja na kutoa huduma za matibabu kuwa bure akifuata  nyayo za Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.

“Suala la matibabu kuwa bure ni muhimu kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kuwa na afya njema waweze kukabiliana na maradhi mbalimbali hatari kwa afya zao.”

''Nikichaguliwa kuwa Rais nakusudia kufuata nyayo za Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, kwa kuifanya sekta ya elimu na afya kuwa bure ili wananchi wafaidike na matunda ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964,'' alisema.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi