loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fella afurahia TMK wanaume kurudi

MENEJA  wa muziki wa kizazi kipya, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amefunguka amefurahi kundi la wanaume (TMK) kurudi kuimba muziki pamoja.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Fella alisema yeye kama kiongozi wao amefurahishwa  na maamuzi hayo  kwani siku zote anatamani  kuona wasanii wake wanafanya kazi pamoja kama ilivyokuwa zamani.

“Mimi napenda kwa sababu mwisho wa siku mashabiki  walikuwa na shauku na kutamani kuona  wanarudi na kufanya kazi pamoja .

“Hata mwenyewe  nimempenda  Juma Nature na Amani Temba kurudi kwenye kazi na kukubaliana kuanza kufanya kazi  na sasa hivi tunawaona wapo mikoani na Rais John Magufuli kwenye kampeni za kuomba kura kwa wananchi,” alisema Fella.

Alisema alikuwa anatamani hata kundi la wanaume halisi warudi kwenye muziki lakini hawezi kuwalazimisha kufanya hivyo kwani maamuzi wanayo wao wenyewe.

“Ni wakati wa kurudi na kukaa pamoja wakubaliane warudi kwenye kazi yao waliyokuwa wanaitegemea kuingiza kipato miaka ya nyuma, wakiona kama ni maisha yao  watarudi na kuanza kufanya kazi pamoja ,“ alisema Fella

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 15 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 15 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...