loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wassira awaombea kura wagombea CCM

WAZIRI mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wassira ameomba wakazi wa Manispaa ya Musoma wawapigie kura wagombea kutoka vyama vyenye ilani ya uchaguzi makini kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Mji wa Musoma katika mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Mara Sekondari, kata ya Nyamatare, wilayani Musoma, mkoani Mara.

"Tukisema mkapige kura, nendeni mkapige kura kwa wagombea na vyama vyenye Ilani ya Uchaguzi. Si kukupigia chama ili mradi ni safari tu ya kwenda kupiga kura. CCM inazo sera zake na ndiyo maana tunawaomba muwapigie kura wagombea wa CCM," alisema Wassira na kuongeza;

"Hatuwezi kumpa mtu kura za urais kwa sababu tu tumekutana njiani. Rais ni Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Majeshi. Tunamuombea kura Rais Magufuli kwa sababu amejaribiwa na ameweza".

Alisema, Magufuli amekamilisha ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa, Mara ndani ya miaka mitatu, na kwamba ujenzi huo ulisimama kwa zaidi ya miaka 40.

 Uamuzi wa kujenga ile hospitali ulianzishwa kwa azimio la chama cha Tanganyika African National Union (Tanu) la mwaka 1974 na likathibitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho mwaka huo huo.

“Hapakuwa na bajeti ya ujenzi, lilikuwa ni suala la kujitegemea. Kwa hiyo, tulianza na michango ya soda ndiyo maana ujenzi wake umechukua muda mrefu kukamilika," alisema Wassira.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi