loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tundu Lissu aahidi neema kwa wakulima kahawa

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lisu amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Kagera kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha wakulima wote wa kahawa wananufaika na zao hilo.

Alisema wakati wa uongozi wake kila mkulima anayelima kahawa ataruhusiwa kuuza mazao yake popote bila kujali kama kuna vyama vikuu vya ushirika au la.

Aliyasema hayo uwanja wa Kayanga Lisu wilayani Karagwe mkoani Kagera katika mkutano wa kampeni kuomba wananchi wamchague awe Rais.

"Wanaolima nyanya, wanaolima ndizi , vitunguu , mihogo viazi hawajawahi kuzuiliwa na kuulizwa wanalipa wapi au wanashamba wapi , lakini kwa nini mkulima wa kahawa anaambiwa ili kahawa yake ipokelewe katika chama cha msingi  lazima awe na shamba la  kahawa , lakini anayekuuliza hajui ulipanda lini, ulitumia mbolea au laha ,anaonekana katika mavuno, nitaondoa hayo yote mkinichagua , kila mtu atauza kwa uhuru anapotaka" alisema

Alidai kuwa, viongozi wa serikali na wa vyama vikuu vya ushirika wanatumika kuwakandamiza wananchi kwa kuwapa bei wanayoitaka bila kujali nguvu  zinazotumika.

"Karagwe na Kyerwa ni wakulima wazuri , kwa upande wangu naona wanavyonyanyasika katika uuzaji wa kahawa ,wakulima wanatumia nguvu kubwa kulima lakini wanalipwa shilingi 1,200 tu, hii sio sawa ,mnaibiwa sana, mimi nikichaguliwa nitatangaza neema kwa wakulima wote wa kahawa na kuwapatia bei nzuri " alisema Lisu.

Mgombea huyo pia aliwaahidi wananchi kuwa atatatua migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiwakumba wananchi kwenye mkoa wa Kagera.

Alisema mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi kwa asilimia 80 hivyo akichaguliwa atachagua mbinu bora ya kukomesha changamoto ya ardhi hivyo amewaomba wananchi wamuchague.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Diana Deus, Bukoba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi