loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Suarez kutua Atletico Madrid

KLABU ya Barcelona imekubali kumuachia mshambuliaji wake Luis Suarez kujiunga na wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga Atletico Madrid.

Suarez alikuwa hatakiwi Barca na klabu hiyo ya Catalan ilikuwa na furaha kumruhusu kuondoka bila hata ada yoyote, lakini kwa sharti la kutojiunga na klabu nyingine yoyote kubwa nchini Hispania.

Tayari mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amekubaliana maslahi binafsi, ikiwemo kupunguziwa mshahara hapo Atletico baada ya kushindwa kwa mpango wake wa kuhamia Juventus kutokana na suala  la hati ya kusafiria.

Mwenyekiti wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu baadae alizuia mpango huo kwa sababu hakutaka kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani wao wa La Liga.

Lakini, baada ya kukutana na wawakilishi wa Suarez, klabu hiyo ilibadili msimamo wake, huku mshambuliaji huyo akitishia kuweka hadharani kwa vyombo vya habari kuhusu malalamiko yake.

Atletico watatakiwa kulipa ada kidogo kiasi cha Euro milioni 4 kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ambacho kitategemea na thamani kama ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Suarez akiwa katika klabu yake hiyo mpya atapata nusu ya Euro milioni 30 kwa mwaka ukilinganisha na ule aliokuwa akilipwa Barcelona.

Uhamisho huo unahitimisha miaka sita ya Suarez kuichezea Barca, ambako alifunga mabao 198 katika mechi 283 alizocheza na alitengeneza `utatu’wa ushambuliaji uliokuwa ukiundwa na Lionel Messi na  Neymar.

Alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya kiasi cha pauni milioni 74 akitokea Liverpool mwaka 2014 na aliwasaidia kushinda mataji manne ya La Liga, manne ya Copa del Reys na moja la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na lile ya Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2015.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amejikuta katika wakati mgumu baada ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi