loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barakah the Prince awaangukia mashabiki

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Baraka Andrew ‘Barakah the Prince’amewaomba mashabiki wake kuipokea kwa mikono miwili video mpya ya wimbo wa Sawa. 

Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kutambulisha video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii alisema ni wakati sahihi kwa mashabiki wake kuchangamkia kazi hiyo.

“Nilikaa kwa muda kidogo bila kuachia video ya wimbo wangu wa Sawa, sasa ipo sokoni nawaomba mashabiki wangu kuniunga mkono, naamini ni kazi bora kwao,”alisema Prince.

Barakah the Prince aliyewahi kutamba na vibao kama Nimekoma, Nivumilie na Siwezi alisema ameachia wimbo pamoja na video baada ya kukaa kwa muda mrefu.

“Siku zote sisi wasanii tuna wajibu wa kuwalinda mashabiki wetu, kwa kuwa bila wao kazi zetu haziwezi kufanikiwa wanatuunga mkono kila tunapotoa wimbo," alisema.

Alisema kwa muda mrefu alikaa kimya kujiandaa ili atoe kazi bora kwa kuwa soko la muziki lina ushindani mkubwa, huwezi kuuza kama nyimbo zako hazitazingatia mahitaji ya mashabiki.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 14 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 14 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...