loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBS yatatua kero Temeke kupitia ‘One Stop Jawabu’

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi jijini Dar es Salaam kupitia maonesho ya ‘One Stop Jawabu’ yaliyoanza Septemba 14, mwaka huu katika Viwanja vya Mbagala Zakheem na kutarajiwa kumalizika Septemba 28, mwaka huu katika viwanja vya Mwembeyanga.

Maonesho hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke ili kusogeza huduma kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali.

Katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Eugenia Kibasa, alisema kupitia maonesho hayo wanahudumia wananchi mbalimbali Temeke wanaofika kujua masuala mbalimbali yakiwamo yanayohusu usajili wa majengo ya biashara kama migahawa, hoteli na mashine za kusaga nafaka.

Wengine ni wenye maduka ya vyakula, vipodozi na ‘supermakert’. 

"Kupitia maonesho haya, tunawapa utaratibu wa kuwawezesha kusajili maeneo hayo, wakitakiwa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao," alisema.

Alisema wananchi wanaelimishwa kuhusu bidhaa wanazoagiza nje ya nchi vikiwamo vipodozi na chakula kuwa wanapaswa kuomba usajili wa bidhaa hizo kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kabla hawajaziingia nchini.

"Tunawaelekeza wananchi kuhusu usajili wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Tunajua kwamba kuna wajasiriamali ambao ili wapate leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS wanatakiwa wapitie SIDO ambao ndiyo wanaowathibitisha kuwa hao ni wajasiriamali wadogo," alisema.

Alisema baada ya kuwa wamethibitishwa na SIDO kwamba ni wajasiriamali wadogo, TBS wanapokea maombi yao na kuwapatia huduma za kuthibitisha bidhaa zao ili kuwapatia leseni ya ubora bila malipo, kwani gharama zao zinalipwa na serikali kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa Kibasa, wanapofika mwaka wa nne wanaanza kuchangia gharama ya ada ya mwaka ya leseni kwa asilimia 25. 

"Ada inaendelea kupanda kwa asilimia 25 hadi mwaka wa saba na baada ya hapo wanatakiwa kuchangia kiasi cha ada kamili ya leseni," alisema.

Ofisa Masoko wa TBS, Mussa Luhombero, alisema wameshiriki maonesho hayo ili kuhamasisha wananchi kusajili maeneo wanayotolea huduma kwa mujibu wa taratibu.

"Tupo hapa kuelimisha wananchi kuhusu utaratibu wa kupata alama ya ubora na kuwahamasisha wauzaji wa vipodozi kuhakikisha wanauza vipodozi vilivyosajiliwa ili kuwaepushia wananchi madhara yanayotokana na matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu," alisema Luhombera.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi