loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiungo wa Simba Gerson Fraga kuikosa Yanga

 TIMU ya  Simba imethibitisha kiungo  wake Brazili Gerson Fraga ataukosa  mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga unaotarajiwa kufanyika Oktoba 18  kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Fraga ataukosa mchezo huo baada ya kumia sehemu ya goti kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara  dhidi ya Biashara United,mechi iliyoisha kwa Simba kuchomoza na ushindi  mnono wa mabao 4-0 katika Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisi za kamapuni ya magazeti serikali (TSN), Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema  majeraha aliyopata Fraga yatamfanya akosekane uwanjani kwa zaidi ya miezi miwili.

“Fraga amepata majeraha kwenye mchezo uliopita na tutamkosa uwanjani kwa zaidi ya miezi miwili ni pengo kwenye kikosi chetu,najua itataumiza kwa namna anavyocheza lakini tutatafuta mbadala kuziba nafasi yake.

Nikiungo mzuri na uwezi kumuelewa kama ujuhi anavyocheza na kuwa msaada kwenye kikosi  itatuumiza sina shaka ataukosa mchezo dhidi ya Yanga.”alisema Fraga

Fraga aliyefungua akaunti ya  ushindi  wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga  kwa kuwafunga Yanga  bao la kwanza dakika ya 20 akimalizia pasi kutoka kwa Clatous Chama kwenye mchezo uliopita wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam (FA) uliofanyika Uwanja wa Mkapa.

pia Manara alisema kwa sasa kikosi chao kinaendelea kufanya mazoezi lengo ni kuhakikisha kwenye mechiinayokuja ya ligi dhidi ya Gwambina FC mashabiki wa Simba wanakuja kufurahia soka la kisasa la pasi nyingi.

“Tunataka kutoa burudani kwa mashabiki wetu,wajitokeze kwa wingi waone burudani kwa kucheza mpira wa kisasa wa pasi nyingi zaidi ya mechi iliyopita “alisema Manara

alisema wanamalengo ya kutetea ubingwa ili waendelee kulinda heshima ni lazima wafanye vizuri kwenye michezo yao kwani safari hii wamejiwekea malengo ya kuonesha makali kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

“kwanza tunahitaji kulinda heshima kwa kufanya vizuri ligi ya ndani ,lakini kimataifa malengo yetu ni kufika  nusu fainali kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu tumejipanaga

safari hii tunaenda na risasi moja hatubahatishi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa tunaenda kufanya makubwa  ”alisema Manara.

Aidha Manara alisema kwa sasa bado wanaendelea kuijenga timu hiyo ifanane na zingine na ndio maana Ofisa mtendaji wa Simba Barbara Gonzalez akiongozwa na mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi  Mulamu Nghambi wametembelea makao makuu ya klabu ya Al Ahly ya Misri kwenda kukubaliana na kushirikiana kwenye maeneo ya biashara.

“Tunajua wenzetu wamepiga hatua tumeenda kujifunza mambo ya ufundi uendelezaji wa wachezaji kwa kuja kujenga kituo cha kukuza vipaji kwa kushirikiana na Al Ahly “
 

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 15 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 16 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...