loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbrazil Simba kuikosa Yanga

TIMU ya  Simba imethibitisha kiungo  wake Mbrazili Gerson Fraga ataukosa  mchezo dhidi ya watani zao, Yanga unaotarajiwa kupigwa Oktoba 18, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Fraga ataukosa mchezo huo baada ya kuumia sehemu ya goti kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara  dhidi ya Biashara United, mechi iliyomalizika kwa Simba kuchomoza na ushindi  mnono wa mabao 4-0 katika uwanja huo.

Akizungumza Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema  majeraha aliyopata Fraga yatamfanya akosekane uwanjani kwa zaidi ya miezi miwili.

“Fraga amepata majeraha kwenye mchezo uliopita na tutamkosa uwanjani kwa zaidi ya miezi miwili, ni pengo kwenye kikosi chetu, najua itatuumiza kwa namna anavyocheza, lakini tutatafuta wa kukava nafasi yake.

Ni kiungo mzuri na huwezi kumuelewa kama hujui anavyocheza na kuwa msaada kwenye kikosi itatuumiza, sina shaka ataukosa mchezo dhidi ya Yanga,” alisema Manara.

Fraga alifungua akaunti ya  ushindi  wa mabao 4-1 wakati Simba ilipocheza dhidi ya Yanga, kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 20 akimalizia pasi ya Clatous Chama katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) uliofanyika Uwanja wa Mkapa Julai 13, 2020.

Pia Manara alisema kwa sasa kikosi chao kinaendelea kufanya mazoezi, lengo ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC Jumamosi ili kuwapa furaha mashabiki.

 “Tunataka kutoa burudani kwa mashabiki wetu, wajitokeze kwa wingi waone burudani kwa kucheza mpira wa kisasa, wa pasi nyingi zaidi ya mechi iliyopita," alisema Manara.

Alisema wana malengo ya kutetea ubingwa ili waendelee kulinda heshima, ni lazima wafanye vizuri kwenye michezo yao, kwani safari hii wamejiwekea malengo ya kuonesha makali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwanza tunahitaji kulinda heshima kwa kufanya vizuri ligi ya ndani, lakini kimataifa malengo yetu ni kufika nusu fainali, kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu tumejipanga.

Safari hii tunaenda na risasi moja hatubahatishi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, tunaenda kufanya makubwa, ”alisema Manara.

Aidha, Manara alisema kwa sasa bado wanaendelea kuijenga timu hiyo ifanane na nyingine na ndio maana Ofisa Mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez akiongozwa na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi,  Mulamu Nghambi wametembelea Makao Makuu ya klabu ya Al Ahly ya Misri kwenda kukubaliana na kushirikiana kwenye maeneo ya biashara.

“Tunajua wenzetu wamepiga hatua tumeenda kujifunza mambo ya ufundi uendelezaji wa wachezaji kwa kuja kujenga kituo cha kukuza vipaji kwa kushirikiana na Al Ahly."

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi