loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtibwa: Yanga hachomoki salama

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar imesema mchezo ujao dhidi ya Yanga ni muhimu kwao kupambana na kupata pointi tatu zitakazowasaidia kusogea juu zaidi na kuepuka presha za msimu uliopita.

Mtibwa itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha wa kikosi hicho, Zuberi Katwila alisema Yanga haina tofauti na timu nyingine yoyote wanaiheshimu na kujipanga ili kuondoka na ushindi.

“Tunaendelea na maandalizi mazuri tukiamini Yanga ni timu nzuri kama tulivyo sisi. Tunajipanga na lengo letu ni kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaotuwezesha kusogea juu,”alisema. 

Alisema mchezo huo unaweza kuwa mgumu, kwani Yanga iko kwenye presha ikihitaji matokeo ya kujiweka pazuri kama ilivyo wao, wote wana lengo moja la kupigania taji la Ligi Kuu.

Katwila alisema bila kujali ni uwanja wa nyumbani au ugenini matokeo kwao yana umuhimu mkubwa na hawataki kurudia makosa ya msimu uliopita yaliyosababisha kuwaingiza katika presha ya kushuka daraja baada ya kufanya vibaya.

Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya saba kwa pointi tano haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi wakiwa wamecheza michezo mitatu na kushinda mmoja na kupata sare mbili.

Timu hiyo ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri. Pia walitoka suluhu dhidi ya Ruvu na kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu ugenini.

Mtibwa mara nyingi imekuwa ikiisumbua Yanga hasa inapokuwa nyumbani kwani msimu uliopita walitoka sare ya bao 1-1. 

Pia, wakata miwa hao wamewahi kuwafunga mabingwa hao wa kihistoria mara mbili kwenye uwanja huo hasa msimu wa 2018/2019. 

Kwa upande wake msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwemo maandalizi ya uwanja na kuwaahidi mashabiki kuwa watawapa raha.

Alisema kiingilio cha mchezo huo kitakuwa kimoja tu cha Sh 10,000  na mauzo ya tiketi yatafanyika kuanzia Jumamosi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 15 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 15 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...