loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea NCCR aahidi kutatua kero ya uchafu

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Nicolas Clinton ameahidi kutatua kero ya uchafu uliokithiri katika kata za Ilala, Jangwani na Mchikichini.

Clinton alitoa ahadi hiyo juzi wakati alipokutana na wananchi wa kata ya Mchikichini kunadi sera zake ambapo pamoja na mambo mengine aligusia namna atakavyoimarisha mazingira bora ya ufanyaji wa biashara.

Alisema kama mazingira yakiwa safi, afya za wananchi zitaimarika na hata biashara zinaweza kufanyika kiurahisi, hivyo akawataka wananchi kumchagua ili kupitia sera yake hiyo mtambuka awasaidie.

Alisema katika kuhakikisha sera yake ya ubora wa mazingira safi inatekelezwa atashinikiza miradi mbalimbali ya miundombinu hasa uboreshwaji wa mitaro na barabara inatekelezwa jimboni humo ili kupitisha maji machafu yanayozagaa mitaani.

Alisema:”Kumekuwa na uzembe katika kulishughulikia suala la uchafu, sasa ninataka kuwahakikishia kuwa nitapambana ili mazingira yote ya jimbo la Ilala yawe safi na salama kwa watu kuishi, kufanya biashara na shughuli nyingine zote.

 

Mfano kumekuwa na mtaro korofi hapa kwa Mpare Mchikichini sijajua ni kwa nini muda mrefu maji yamekuwa yanatuama hapa, sasa ninachowaomba mnichague ili nikabiliane na mambo yote korofi kwenu.”

Alisema atawapatia vitambulisho vya mjasiriamali wafanyabiashara wasiokuwa na uwezo wa kuvinunua huku akiahidi kuwachongeshea meza za kufanyia biashara wafanyabiashara wote hasa wanaofanyia biashara zao kwenye masoko.

Pia alisema ataweka mfumo shirikishi wa utozaji wa kodi kwa wafanyabiashara wa Ilala kwa kuwa haridhishwi na namna kodi zinavyotozwa jimboni humo kwa sasa.

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi