loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea CUF kuondoa adha korosho kuuzwa kwa mkopo

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mkinga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Nuru Bafadhili amesema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza atahakikisha anawasaidia wakulima wa korosho kuondokana  na adha ya kuuza zao hilo kwa mkopo.

Ahadi hiyo aliitoa juzi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Duga sigaya wilayani humo. Alisema wakulima wamekuwa wakipata adha ya kucheleweshewa malipo yao hali inayowafanya kuishi maisha magumu.

Alisema atahakikisha anamaliza kero iliyopo kwa wakulima wa korosho ya kuchukuliwa mazao yao na kuweka kwenye ghala bila ya kulipwa kwa wakati.

"Nichagueni mimi mgombea wa CUF nikawe mtetezi wenu, haiwezekani wakulima walime kwa shida halafu hata kuuza mazao yao iwe ni kero  ni lazima tuweke utaratibu mwingine wa malipo kila unapopeleka mazao,"alisema.

Hata hivyo alisema atasimamia mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na walemavu inatoka kwa wakati ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato chao.

Alisema kama wanamkinga wanahitaji maendeleo ya kweli hawana budi kumchagua yeye mgombea wa CUF ambaye anajua kero zilizopo katika wilaya hiyo.

"Niwaombe wananchi acheni udalali katika kuchagua mwakilishi wenu lazima mkubali mabadiliko na kuchana na mazoea ikiwa mnataka maendeleo ya kweli katika jimbo hili,"alisema.

Hata hivyo kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jamal Nassor aliwataka wananchi kuachana na ubaguzi bali wachague kiongozi ambaye ataweza kuwapelekea maendeleo.

"Kipindi hiki ambacho kama wananchi hawatakuwa makini wanaweza kubaguana kutokana  na sera za baadhi ya wanasiasa wasio na dhamira njema, niwaombe hakikisheni mnakuwa wamoja na msiruhusu kubaguliwa,"alibainisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Mkinga, Juma Zuber alisema kata hiyo imeweza kupelekewa Sh bilioni 1.8 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Hivyo aliwataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchagua mgombea wa udiwani wa CUF kwani ndio wameweza kusaidia kuleta maendeleo.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Amina Omari, Mkinga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi