loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cole afichua ugumu wa Man Utd kusajili

ANDY Cole anaamini Ole Gunnar Solskjaer ana kazi ngumu kushawishi wachezaji wenye viwango kusajili Manchester United na ameionya klabu yake hiyo ya zamani kuhusu kufanya usajili kwa jazba na presha. 

Zikiwa zimesalia siku 10 dirisha la usajili kufungwa, makocha wa timu mbalimbali wameendelea kufanyia kazi mapungufu na kuboresha vikosi vyao.

Wakati ikionekana kama kutakuwa na wachezaji watatu watakaosajiliwa kabla ya dirisha kufungwa, kuna matumaini angalau mmoja anaweza kukisaidia kikosi cha Solskjaer.

Aidha, Cole anaamini kuwa mnorway huyo ana kazi ngumu kwenye usajili kutokana na mafanikio ya Manchester City na Liverpool na wachezaji wanaona uhamisho wa Old Trafford hauwanufaishi. 

Aliiambia Goal:  "Kujaribu kuifikia Liverpool na Manchester City wanatakiwa waache kusajili kwa kujiimarisha wenyewe, wakati wakijaribu kuwa na aina moja ya wachezaji.”

"Wakati Manchester United wanatawala, wachezaji wote wazuri walitaka kuja Man United na walitaka kuja kwa sababu walikuwa na nafasi ya kushinda mataji, ni hivyo tu.”

"Unapokuwa huna nafasi ya kushinda huwezi kusema utakwenda Man United kama Liverpool au Man City zinakutaka. Unakwenda kwenye moja ya klabu unazoweza kushinda kitu.”

"Huo ndio ugumu anaokutana nao Ole kwa sasa, kusema nadhani unaweza kusajili Manchester United badala ya Man City au Liverpool kwa sababu tunajenga timu ya miaka miwili au mitatu ijayo kisha baada ya hapo tunaweza kushinda ubingwa wa ligi, kwangu momo kama ni mchezaji nitafikiria kwanza, kwa miaka miwili au mitatu?”

"Au nataka kuanza kushinda mataji sasa na kisha ndani ya miaka miwili au mitatu niamue… kushawishi mchezaji aliye kwenye kiwango kwa sasa kusajili timu kisha akae miaka mitatu ndio ashindanie ubingwa haiwezekani.”

Jadon Sancho anabaki kuwa mchezaji anayewaniwa kwa udi na uvumba na Solskjaer lakini Dortmund bado imeshikilia msimamo wake kwamba mchezaji wao huyo wa kimataifa wa England anabaki kwao. 

TIMU za Liverpool na Chelsea jana zilibanwa mbavu baada ya ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi