loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchambuzi Kimataifa: Tanzania ina mazingira bora ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

MWANATAALUMA wa masuala ya usalama, Profesa Richard Andes,  amesifu amani iliyopo nchini kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Prof Andes amesema hayo yamewezekana kutokana na  kila chama kukubali na kusaini fomu za maadili zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kuelekea uchaguzi huo,  ikiwa inalenga kuwapo kwa amani kabla na baada ya upigaji wa kura.

Kila chama chenye usajili wa kudumu kilitia saini makubaliano hayo yanayolenga kipindi hiki chote cha kampeni  pamoja na siku ya kupiga kura.

“ Ninafurahi kutambua kuwa kila chama na kila mgombea  alisaini fomu za maadili. Ninafurahi kuona kuwa kampeni zinafanyika kwa utulivu na amani,” amesema.

NEC ilitoa fomu za maadili kwa lengo la kuhakikisha kuna usawa, maelewano, pamoja amani wakati wote mchakato wa uchaguzi mkuu ukiendelea.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi