loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Esther Matiko atambia maendeleo ya kisekta Tarime

MGOMBEA anayetetea kiti cha ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema), Esther Matiko amesema maendeleo ya kisekta aliyowaletea wakazi wa jimbo hilo yanatosha kuwashawishi kumwongezea kipindi kingine cha miaka mitano ya kuwawakilisha bungeni.

Matiko alisema licha ya kukabiliwa na kesi kadhaa mahakamani jijini Dar es Salaam, muda wote alikuwa mwepesi wa kupokea na kushughulikia kwa mafanikio na kutafuta ufumbuzi wa matatizo jimboni humo.

Alisema katika kipindi chake cha miaka mitano ya ubunge Tarime Mjini alielekeza nguvu kubwa katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii, hasa miundombinu ya barabara, afya, elimu, umeme na maji.

“Wakati nachaguliwa kuwa mbunge mwaka 2015 barabara nyingi katika jimbo hili zilikuwa hazipitiki, lakini sasa hivi barabara za mitaa yote 81 zimezibuliwa kwa kiwango cha changarawe, makaravati na madaraja yamejengwa.

Baadhi ya barabara zikiwemo za Bomani zimewekewa lami,” alisema. Kuhusu afya, Matiko alisema katika kipindi chake cha uongozi serikali imepeleka x-ray mbili mpya kwa ajili ya huduma za kitabiku katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Pia serikali imefanya ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na ujenzi wa maabara za kisasa, japokuwa bado kuna changamoto za dawa, vifaa tiba, watumishi na huduma ya maji.

Kwenye sekta ya elimu, Matiko alisema alipoingia madarakani alikuta shule nyingi ziko hoi, lakini kutokana msukumo wake nyingi zimeboreshewa miundombinu.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Christopher Gamaina

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi