loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wamachinga waonya wanasiasa kugeuza vitambulisho mitaji

WAFANYABIASHARA biashara ndogo (wamachinga) kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekemea wananasiasa wanaobeza vitambulisho vya wajasiriamali kwa kutaka kuwageuza mtaji wa kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Wakitoa ushuhuda namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyosaidia kuboresha shughuli zao, walisema vitambulisho vimewajengea heshima na kuwaondolewa bugudha walizokuwa wakikumbana nazo kabla Rais John Magufuli kuanzisha utaratibu huo.

 Wakizungumzia manufaa ya vitambulisho, wamachinga na wajasirimali wanaouza bidhaa mbalimbali stendi kuu na soko la jioni katika eneo la Nyerere Square jijini Dodoma, walisema vimewapa heshima na kuwataka wanasiasa wasiwatumie kama mtaji wa kisiasa wa kupata kura.

Miongoni mwa waliozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, walipinga kauli ya mgombea mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu kwamba wameibiwa na kudhulumiwa kupitia vitambulisho hivyo.

Wakitoa tamko lao, walisema mgombea huyo akiwa katika mkutano wa hadhara Isaka wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga, alikejeli na kupotosha kwamba vitambulisho vya ujasiriamli ni wizi na kwamba wamachinga wameibiwa, wamedhulumiwa kwa kuvinunua kwa Sh 20,000.

Mwenyekiti wa Soko la Jioni Nyerere Square, Baraka Mlisho alisema wanasiasa wasiwatumie wamachinga kutafuta kura na kuwafanya mtaji wa kisiasa kwani vitambulisho hivyo vimewapa heshima kubwa na kuondoa ushuru waliokuwa wakitozwa.

Alisema kabla ya kupata vitambulisho hivyo, walikuwa wakitozwa sh 1,000 kwa siku sawa na sh 30,000 kwa mwezi au Sh 360,000 kwa mwaka.

Alifafanua kuwa hawakulazimishwa kulipia vitambulisho hivyo na kwamba walikuwa wakivilipia kadiri ya uwezo huku wakilipa kwa awamu.

Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga mkoani Dodoma, Bruno Mponzi alisisitiza kuwa hawajaibiwa wala kudhulumiwa na wana imani na kiongozi wa na kiongozi wa hicho aliyeamua kuwapa vitambulisho hivyo ambavyo vimewapa heshima kubwa.

“Wasitafutie kura kwa wamachinga, kwani Rais Magufuli amewathamini wamachinga na wanaahidi kwamba ifikapo Oktoba 28, watampigia kura na kauli yao ni ‘Wamachinga na Magu miaka mitano tena,” alisema.

Alisema wanasiasa wanatakiwa kujikita katika kunadi sera za vyama vyao badala ya kuwatumia wamachinga na wajasirimali kama mtaji wa kisiasa au kutegemea kwamba watapewa kura za huruma.

Kwa mujibu wa makamu mwenyekiti huyo wa wamachinga, vitambulisho hivyo waliomba wenyewe walipokutana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa (Tamisemi) Mei 21, 2017 wakaomba kutambuliwa na ndipo Rais Magufuli alikubali ombi hilo na kuwaandalia vitambulisho.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi