loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Solskjaer awataka wachezaji United kujituma

KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amewataka wachezaji ambao hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza kuendelea kujituma mazoezini ili wamshawishi kuwatumia katika michezo ijayo.

Solskjaer alisema kama miongoni mwao watabweteka hatowatumia hata kama watachukia kwa sababu yeye kazi yake ni kufundisha mpira na sio kuwafanya wachezaji wawe na furaha.

“Wachezaji huwa na furaha kama wanacheza vizuri na kupata ushindi katika mechi, lakini pia sio kazi yangu kuwafanya wawe na furaha maana kazi yangu ni kuchagua wachezaji bora ili waweze kunipatia matokeo bora,” alisema Solskjaer.

“Ni kazi yao sasa kufanya mazoezi kwa bidii ili waendelee kuwa bora na wakifanya hivyo wasubirie kuchaguliwa sasa,”.

Miongoni mwa wachezaji wanaolengwa ni mshambuliaji Jesse Lingard, ambaye hakucheza mechi ya kwanza ya ligi msimu huu dhidi ya Crystal Palace, ambapo taarifa zinaeleza kuwa huenda akaondoka Old Trafford kwa sababu wakala wake anafanya mazungumzo na klabu kadhaa nchini England na sehemu zingine barani Ulaya.

Wengine ambao rungu la kocha huyo limewadondokea ni mlinda mlango Sergio Romero, walinzi Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo na Andreas Pereira ambao hawakuwepo katika mchezo wa Kombe la Carabao dhidi ya Luton.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi