loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DED akanusha madai ya Lissu

MKURUGENZI wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya (pichani) amekanusha kauli ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lisu aliyoitoa katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi Mwanza, akisema Mgombea Urais wa CCM, John Magufuli amewaita Jijini Dodoma wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mkuu 2020.

Wakurugenzi wa majiji, manispaa na halmashauri za wilaya ni wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi yaliyopo katika halmashauri zao .

“Nakanushe kwa uzito mkubwa, hatujawahi kualikwa wala hatujakwenda Dodoma juzi ... nimewasiliana pia na wakurugenzi wenzangu hakuna kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma.

Fikirieni umbali mrefu uliopo kati ya Sumbawanga na Dodoma kwa uharaka huo wa safari, labda kama ningesafiri kwa ungo. Zipuuzeni kauli hizi, tupo vituoni tukitekeleza majukumu yetu. Wiki yote iliyopita hadi leo (jana) nimekuwa nikipokea maombi ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,”alisisitiza.

Mtalitinya alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanahabari mjini hapa jana. Aliwataka wagombea katika nafasi mbalimbali, kuachana na tabia ya kutoa takwimu ambazo sio sahihi, kwani kufanya hivyo ni upotoshaji.

“Kwa wagombea kutoa taarifa za uzushi au uongo katika kampeni zao za uchaguzi ni kosa la maadili, kama wana malalamiko yoyote yale wayawasilishe katika kamati za maadili na kamati za rufaa,”aliongeza.

Aliwataka wagombea kufanya kampeni zao za uchaguzi, wakijiepushe na lugha za uchochezi zisizo za kistaarabu, kwamba kwa kufanya hivyo kutasasabisha uvunjifu wa amani.

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi