loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera SMZ kukamilisha jengo la tatu la abiria

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein juzi alifungua jengo jipya la abiria na eneo la maegesho ya ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (Terminal III) lililopo Kiembesamaki, Unguja.

Dk Shein alieleza kuwa kufunguliwa kwa jengo hilo jipya la uwanja huo ni miongoni mwa hatua za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015-2020 Ibara ya 94 kifungu (a) ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Awamu ya Saba iliagizwa kutekeleza ujenzi huo.

Ujenzi huo wa jengo hilo ulianza Februari 2011, lakini ulikumbwa na changamoto mbalimbali ambazo SMZ ilizitatua na kufikia mafanikio hayo ya kulizindua jengo hilo.

Gharama za awali zilikuwa Dola za Marekani milioni 70.4, lakini mradi huo mpaka kukamilika kwake umegharimu dola za Marekani milioni 128.75.

Kwa maelezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafiri, Mustafa Aboud Jumbe Mwinyi, jengo hilo lina ukubwa wa mita za mraba 25,000, milango minne ambayo kitaalamu inaitwa mikonga mikubwa na midogo ya kupitia abiria wanaoondoka au kuwasili, na barabara ya kurukia ndege yenye ukubwa wa mita za mraba 36,000.

Pia kuna kumbi za abiria wa ngazi mbali mbali na kuna eneo la maegesho ya gari lenye ukubwa wa mita za mraba 8,818 ambalo lina uwezo wa kuegesha gari 214 kwa wakati mmoja.

Tungependa kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanikisha mradi huo mkubwa ambao kimsingi utaleta manufaa makubwa, kama alivyosema Rais Shein kwamba kuwa na miundombinu bora ya kisasa ya usafiri ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa ndani ya nchi kupitia vyanzo vya ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa manufaa hayo ni kuwa jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.6 kwa mwaka ambalo litamudu ongezeko la wageni hasa watalii ambao wamekadiriwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kufikia 850,000 kwa mwaka kutoka idadi ya mwaka uliopita Desemba, 2019 walikuwa 538,000.

Tunampongeza Rais Shein na serikali yake kwa kusimamia maendeleo haya makubwa visiwani Zanzibar ambayo yataendelea kuwa kichocheo kikubwa katika sekta ya usafiri wa anga na pia kuchochea na kukuza sekta nyingine zikiwamo za utalii, biashara na uhusiano wa kimataifa.

Sisi tunaamini kuwa kufunguliwa kwa jengo hili jipya ni kufungua masoko mengine ya utalii kwa watalii wengi kutembelea Zanzibar.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi