loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Spurs yaiondoa Chelsea kwa penalti

MASON Mount alikosa penalti muhimu wakati Tottenham ikiiondoa Chelsea kwa penati 5-4 na kutinga robo fainali ya Kombe la Carabao.

Timu hizo zilifikia hatua ya kupigia matuta hayo baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya kufunga bao 1-1 katika mchezo huo. Jumla ya penalti tisa zilifungwa kabla Mount kujipanga kwa ajili ya kupiga penalti ya 10, lakini kiungo huyo wa England juhudi zake hazikuzaa matunda baada ya penalti yake kugonga mwamba na kupaa nje.

Chelsea ndio ilitawala mchezo huo na ilitawala kipindi cha kwanza na ingizo jipya, Timo Werner alifunga bao la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo akifunga pembeni kabisa ya lango.

Hata hivyo, Spurs walijibu mapigo baada ya mapumziko na walishambulia lango la wapinzani wao kama nyuki, lakini kipa wa Chelsea alijitahidi na kuokoa michomo mbalimbali iliyoelekezwa kwake.

Kikosi cha kocha Jose Mourinho kilipata zawadi dakika saba kabla ya mchezo kumalizika wakati krosi ya Mhispania Reguilon ilipogonga mguzo ya nyuma ya kumkuta Erik Lamela aliyefunga akiwa ndani ya boksi.

Baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo haukuongezwa muda na moja kwa moja hatua ya penati ilifuata na Mount ndiye pekee aliyekosa kufunga.

Kocha wa Spurs Mourinho alionekana kama hakutilia maanani mchezo huo kabla, ambapo alisema nguvu zao wanazielekeza katika michuano ya Ligi ya Ulaya kwani fedha zinazotoka kitoka kwao ni muhimu. Ratiba imeibana timu hiyo kwani itacheza mechi tatu ndani ya siku nane.

TIMU za Liverpool na Chelsea jana zilibanwa mbavu baada ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi