loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachambua changamoto machapisho ya kitaaluma

IMEBAINIKA kuwa shughuli za uchapishaji wa majarida, matini na machapisho ya kitaaluma ambazo ndio uti wa mgongo wa misingi ya kitaaluma zimekuwa na changamoto kiasi cha kuwakosesha baadhi ya wahusika haki zao za msingi.

Hayo yalijitokeza katika majadiliano miongoni mwa washiriki wa warsha ya siku tano kuhusu uandishi wa makala, machapisho na matini mbalimbali za kitaaluma inayoendelea katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dar es Salaam.

Akiwasilisha mada katika warsha hiyo, Profesa Mugyabuso Mulokozi alisema uchapishaji wa kazi mbalimbali za kitaaluma ni kazi ngumu ambayo inahitaji umakini na muda mwingine hata muda wa ziada ili kuhakikisha upatikanaji kazi za kitaaluma zinazokidhi ubora.

“Kulegalega kwa shughuli za uchapishaji wa majarida ya kitaaluma katika taasisi nyingi za elimu ya juu kunatokana na changamoto za kiuendeshaji,” alisema.

Alisema katika mchakato wa kufanikisha jambo lolote hususani uchapishaji lazima kuna gharama zinahusika hivyo lazima masuala yote kuhusu haki za wahusika kwenye mnyororo wa uchapishaji ziangaliwe ili kuwapa motisha ya kazi waifanyayo.

Kwa upande wake, mshiriki wa warsha hiyo, Mhadhiri Evaristo Mtitu wa Kitivo cha Elimu chuoni hapo alisema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya vyuo nchini kuwa na mifumo ambayo haikubali kazi za kitaaluma kutoka taasisi nyingine za elimu ya juu, hivyo kuwakosesa haki za upandaji madaraja kitaaluma.

“Kumekuwa na changamoto za hadhi ya machapisho ya kitaaluma ya ndani na hata baadhi ya taasisi za elimu ya juu kutotambua au kukubali mwanataaluma kuchapisha kwenye baadhi ya majarida mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuamini ubobevu wa wanataaluma wanaohusika katika mchakato mzima,” alisema

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Vincent Mpepo, OUT

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi