loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usipoteze haki kwa kuuza kadi ya mpigakura

OKTOBA 28, mwaka huu watanzania watapiga kura kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa miaka mitano nchini katika ngazi ya urais, ubunge na madiwani baada ya wananchi wenye umri unaoruhusiwa kupiga kura kupata vitambulisho, kuhakikiwa na baadaye kutolewa kuandikwa katika daftari la kupiga kura kuhakikisha wako tayari kwa kuchagua viongozi.

Kupiga kura ni haki ya msingi ya mwananchi kidemokrasia  katika kuchagua viongozi watakaoongoza kwa ajili ya kujiletea maendeleo baada ya wagombea katika ngazi zote kupiga kampeni kwa kueleza wananchi kile watakachofanya baada ya kuchaguliwa hivyo kufanya uamuzi ulio sahihi.

Kati ya vifaa muhimu vitakavyokuwezesha kupiga kura ni kitambulisho cha mpigakura, lakini kuna baadhi ya watu wanatumia vibaya haki hiyo kwa kwenda kununua vitambulisho kwa lengo ovu la kusababisha watu kutopiga kura.

Lakini licha ya kupiga kura, kitambulisho hicho kimekuwa kikitumika katika masuala mbalimbali yanayohitaji utambulisho wako hivyo unaweza kuingia matatizoni iwapo kitatumika vibaya.

Mwito wangu kwa wanawake ambao ndiyo wapigakura wengi nchini wakahakikishe wanatunza vitambulisho hivyo na kamwe wasikubali kuviuza au kutumia kupewa mikopo na watoaji mikopo kuchukua vitambulisho kama dhamana.

Hakuna thamani yoyote ya fedha inayoweza kuwa sawa na kitambulisho chako unachotumia katika kutimiza haki yako ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi watakaoweza kukuongoza kwa mujibu wa sheria.

Tahadhari mnapoona watu wanaotaka kununua vitambulisho au kutaka kuchukua vitambulisho kwa lengo la kuwapatia mikopo kutoa taarifa katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe kwani ni kinyume cha sheria.

Hivi karibuni, Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya alitoa onya kwa  wananchi wanaouza kadi zao za mpigakura kwa siri kwani ni kinyume cha sheria na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema kuwa zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya wananchi wameanza kuuza kadi hizo kisirisiri na kuwa ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni mali ya aliyejiandikisha kwenye daftari la mpigakura.

Kutokana na kauli hiyo, ni vyema wananchi na wanawake kwa ujumla kuhakikisha wanatunza kadi zao za kupigakura na kuhifadhiwa kwa umakini ili wazitumie kama ilivyokusudiwa ili kuepuka kuchukuliwa hatua pale inapobainika .

Ikumbukwe kuwa kumpa mtu mwingine kadi yako na ikihifadhiwa au kutumika vibaya ni ngumu kukwepa lawama hizo au ukitaka kuitumia kupata kadi nyingine itasababisha changamoto kwa kudanganya umma kwa kudai imepotea lakini kumbe kuna mtu amehifadhi kadi hiyo, kitendo hicho ni hujuma na kinyume cha sheria.

Wananchi badilikeni na kuona umuhimu wa haki hiyo ya msingi na msikubali  wanasiasa wenye siasa chafu kuchukua au kununua kadi zenu au kuzichukua kadi hizo wakati huu wa Uchaguzi Mkuu.

KATIKA kipindi cha miezi michache iliypopita, dunia ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi