loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuwakatae wagombea wenye vitisho, matusi

MWISHONI mwa wiki, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, alikutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu na ushiriki wa wanawake katika mchakato wa uchaguzi huo.

Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, mada iliyotolewa na Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Women Fund Tanzania, Profesa Ruth Meena ilihusu mtazamo wa wanawake katika kampeni zinazoendelea nchini na ushiriki wao kwenye mchakato mzima wa uchaguzi ndani ya vyama na nje.

Profesa Meena alipowasilisha mada hiyo, alisema wanawake wana maeneo sita ambayo hawajapendezwa nao katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikiwamo rushwa ya ngono na baadhi ya wagombea kutumia lugha za matusi, zinazowadhalilisha wanawake.

Alisema pamoja na dhamira nzuri zinazojionesha kwenye vyama vya siasa kupitia ilani, bado vinapaswa kutambua kuwa Tanzania ni nchi huru, yenye amani na maendeleo na kueleza kuwa bila ushiriki wa wanawake, mambo hayo hayatadumu.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Jaji Mutungi ambaye alitumia hadhira hiyo kuonya na kukemea wagombea wanaotumia vitisho na vurugu kutaka watu waingie barabarabani kuandamana endapo hawatatangazwa wameshinda katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Binafsi naungana na viongozi hawa kupaza sauti kuwa, wagombea wenye viashiria vya kutaka nchi iingie kwenye vurugu na amchafuko eti kwa sbabau ya kutafuta haki, tuwakatae ili kuwaonesha kuwa Watanzania tumestaarabika, tunayaona na tuna utashi wa kujua jema na baya.

Naamini katika falsafa isemayo hakuna haki bila wajibu. Wakati tunapotafuta haki, tunapaswa kufahamu upo wajibu wa kufanya ili kuipata haki kwa njia inayoleta matokeo mazuri kwa jamii nzima. Suala la vitisho, matusi, kejeli na vurugu, tusilipe nafasi katika na watu wa aina hii, tuwapuuze kabisa kwani hawana nia njema na Taifa hili.

VYAMA vingi vya michezo ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi