loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea urais Chadema ajitoa

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuwa Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chadema, Said Issa Mohamed amejitoa na wanamuunga mkono Mgombea Urais kupitia Chama Cha ACT Wazalendo, Seif Sharif Hamad.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema jana Dar es Salaam kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliketi juzi kwa dharura kujadili masuala ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu na kuridhia kuwa na ushirikiano.

"Kamati Kuu ya Chadema imeketi jana (juzi), tumezungumzia mienendo ya uchaguzi tumeridhia na kuamua kumuunga mkono Mgombea Urais Zanzibar wa ACT-Wazalendo, Seif Sharif Hamad, na mgombea wetu Ndugu Said ameridhia na anajitoa kwenye mchakato, utaratibu wa kujitoa kwake anaufanya,"alisema Mbowe.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Kamati Kuu ya Chadema inaendelea kuunga mkono wagombea wa vyama vingine vya upinzani wanaokubalika, wa ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali.

Aliiagiza kamati ya ufundi ya chama hicho, kuketi kuangalia majimbo na kata ambazo wagombea wa vyama vingine wanaopenda ushirikiano huo, wanakubalika ili wawaunge mkono.

"Tumechoka kupokea barua kutoka kwa Msajili wa Vyama na NEC kuhusu suala la kushirikiana, kuungana mkono ni utashi binafsi, halihitaji masuala ya sheria, ni jambo la kijamii kumuunga mkono mwingine anayekubalika,"alisema Mbowe.

Kuhusu vyama vingine kumuunga mkono mgombea urais  wa Chadema  upande wa Tanzania Bara, ikiwemo chama cha ACT-Wazalendo, alisema jambo hilo hawezi kulizungumzia, kwa kuwa yeye si msemaji wa chama hicho.

Alisema kwamba chama chenyewe kinaweza kusema, lakini huo ni uamuzi wao na si lazima.

"Siwezi kumsemea mgombea urais wa ACT-Wazalendo wa Tanzania Bara, Bernard Membe au chama chake kuhusu kumuunga mkono mgombea wetu, kwa vile sisi tumemuunga wao kule Zanzibar, kama wataona ni vyema watafanya uamuzi wenyewe, ni suala au jambo la hiyari, hakuna kulazimishwa,"alisema Mbowe.

Akizungumzia uchaguzi huo, Mbowe alisema kwamba watakubali matokea tu iwapo haki itatendeka.

Alitaja mambo manne yatakayofanya Chadema ikubali matokeo kuwa ni: Mawakala wao walioidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutonyimwa fursa ya kuapishwa, mawakala hao kutozuiwa kuingia vituoni, kupewa nakala za matokeo ya upigaji kura vituoni na kuhesabu kura za matokeo kwenye vituo husika.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Na Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi