loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tushirikiane kukomesha ukatili kwa wasichana

JUZI katika gazeti hili tulichapisha habari za kusikitisha za mabinti 48 wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kushindwa kurejea shuleni, baada ya kipindi kifupi cha mapambano dhidi ya janga la Covid-19. Mbaya zaidi ni kuwa 17 kati yao, walithibitishwa kuwa wajawazito, hivyo kupata mimba za utotoni.

Taarifa hiyo ambayo ilipatikana wakati wa mkutano wa kujenga uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa majanga kama Covid 19, mafuriko ili kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya vitendo vya unyanyasaji, inadhihirisha kwamba taifa bado lina safari ndefu ya kuhakikisha usalama wa mabinti.

Ukiangalia taarifa hiyo, unaona kwamba wanafunzi waliopata ujauzito ni wastani wa wasichana nane kwa kila shule ya sekondari.

Hii haikubaliki. Kuna kila sababu ya kuangalia kilichotokea katika shule hizo na vijiji wanakotoka wanafunzi hao ili kujua sababu zilizosababisha maafa hayo na kuanza kuchukua hatua za kuzuia na kuondoa.

Haiwezekani katika akili ya kawaida jambo hilo kuonekana la kawaida, hasa linapogusa shule sita za sekondari za eneo moja.

Hatusemi kwamba kuna uzembe katika mafunzo ya afya ya uzazi kwa shule za sekondari za Chipanga, Kigwe, Bahi, Mpamantwa na Ibihwa. Lakini, pia hatuwezi kukwepa ukweli kuwa wazazi na walezi tuna kila sababu ya kulaumiwa kwa kutowasaidia mabinti hao kuendelea na masomo kwa kukabili changamoto zilizopo.

Kwa idadi hii ya wanafunzi katika eneo moja dogo, ipo haja ya kuweka mradi wa majaribio, baada ya kufanyika kwa mang’amuzi juu ya sababu ya idadi kubwa ya mabinti kutorejea shule na wengine kukutwa wajawazito.

Tuasema hivyo kwa sababu Covid-19 ilikuwa ya miezi mitatu. Je ingelikuaje kama ingekuwa miezi sita au mwaka? Kwa kujua nini hasa kimevurugika katika mazingira wanayoishi vijana wetu, hatuwezi kujua tuwasaidiaje, kwani kama ni sheria ni kali, adhabu ya miaka 30 au kifungo cha maisha si kitu kidogo.

Lakini, watu wanapoendelea kuvunja sheria, ipo haja ya kuangalia makandokando. Swali la kwa nini wastani wa wasichana wanane kwa kila shule ya sekondari wilaya ya Bahi, kuendelea na masomo baada ya Covid-19 na kati yao wasichana 3 lazima lijibiwe.

Kutokana na haya yote, tunaitafadhalisha jamii kutambua kuwa ina jukumu la kuhakikisha ulinzi kwa wasichana dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, kudhuriwa au kukwamisha ndoto zao za kusonga mbele katika ustawi wake na wa jamii inayomzunguka.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

1 Comments

  • avatar
    Patrick kang'anga
    10/01/2021

    Asante kwakunifikishia habiri nilipo Asante Sana.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi