loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Utafiti wampa ushindi Magufuli asilimia 82

RIPOTI ya utafi ti kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu ijulikanayo kama “Tanzania Yaamua 2020” imebainisha kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ameongoza kwa asilimia 82.

Utafiti huo umefanywa na Kampuni ya Utafiti ya RhemaSoft ya Ghana ambayo mtafiti wake, Nicholas Amoako amesema umefanywa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia vigezo na maadili ya utafiti Tanzania.

Amoako alisema kwa upande wa Tanzania Bara, Rais Magufuli ameongoza kwa asilimia 82 akifuatiwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu aliyeongoza kwa asilimia 16.

Mgombea kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe ametajwa kushika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia moja huku vyama vingine vikigawana asilimia moja.

Kwa upande wa Zanzibar, utafiti umeonesha Rais Magufuli ameongoza kwa asilimia 75 akifuatiwa na Lissu asilimia 22 huku Membe akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia mbili na vyama vingine vina asilimia moja.

Mtafiti huyo alieleza kuwa kwa Tanzania Bara, Rais Magufuli ameonekana kung’ara katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, mikoa ya Magharibi, Simiyu na Katavi huku Lissu aking’ara zaidi Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Upande wa Zanzibar, Rais Magufuli ameonekana kung’ara Mjini Magharibi, Mkoani pamoja na maeneo mengine, wakati Lissu ameonekana kuongoza Kaskazini na Kusini Pemba.

Kwa upande wa wagombea urais Zanzibar, alieleza kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi ameonekana kuwa atashinda kwa asilimia 69, Maalim Seif Sharif Hamad wa ACT-Wazalendo ametajwa kuwa atashinda kwa asilimia 29 huku wagombea wa vyama vingine wakitajwa kwa asilimia mbili.

Dk Mwinyi ameonekana kung’ara zaidi katika maeneo ya Mjini Magharibi, Mkoani pamoja na maeneo mengine wakati Maalim Seif ameonekana kung’ara zaidi Kaskazini Pemba.

Mtafiti huyo alisema washiriki waliohojiwa kutoka Bara na Visiwani ni 27,884 ambao kati yao wanawake ni 16,026 ambao ni sawa na asilimia 57 na wanaume ni 11,858 sawa na asilimia 43.

“Kati ya waliohojiwa washiriki waliosajiliwa kupiga kura ni asilimia 92,” alieleza mtafiti huyo wa RhemaSoft.

Akifafanua zaidi, alibainisha kuwa kutoka Bara washiriki walikuwa ni 19,380 ambao wanawake ni 11,434 sawa na asilimia 59 na wanaume ni 7,946 ambao ni sawa na asilimia 41.

Kwa Zanzibar, alisema jumla ya washiriki ni 8,504 ambao kati yao wanawake ni 4,592 sawa na asilimia 54 huku wanaume wakiwa 3,912 sawa na asilimia 46.

Akizungumzia kuhusu mchanganuo wa washiriki hao 27,884, Amoako alibainisha kuwa waliohojiwa wenye umri kati ya miaka 18 hadi 28, idadi yao ni 10,596 ambao ni sawa na asilimia 38.

Alitaja waliohojiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 29 hadi 39 ambao idadi yao ni 6,692 sawa na asilimia 24; kuanzia miaka 40 hadi 50 waliohojiwa ni 5,019 sawa na asilimia 18, na kuanzia miaka 51 hadi 61 waliohojiwa ni 3,625 sawa na asilimia 13 na zaidi ya miaka 62 wamehojiwa watu 1,952 (7%).

Alisema kuwa kati ya washiriki hao waliohojiwa kutoka Bara ni 19,380 ambao kati yao wenye miaka 18 hadi 28 ni 7,946 ambao ni sawa na asilimia 41; miaka 29 hadi 39 waliohojiwa ni 5,233 sawa na asilimia 27; miaka 40 hadi 50 waliohojiwa ni watu 2,713 sawa na asilimia 14; miaka 51 hadi 61 idadi yao ni 1,938 sawa na asilimia 10 na kwa upande wa zaidi ya miaka 62 waliohojiwa ni 1,550 sawa na asilimia nane.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi