loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaume epukeni mikunjo usoni kwa lishe bora

UNAWEZA kufi kiri mwanaume hahitaji vidokezo vya urembo. Ukweli ni kwamba ikiwa unajali afya ya ngozi yako, nywele zako na mwili wako, basi unahitaji kuwa na kanuni kidogo za urembo.

Kwa vidokezo hivi rahisi vya urembo kwa wanaume, unaweza kuufanya mwili wako uwe na furaha bila kufanya kazi nyingi. Katika safu yetu leo tutazungumzia jinsi ya kupunguza mikunjo usoni.

Kwa kuongezea ili kuifanya ngozi kuwa na unyevu, lishe itasaidia kupunguza mikunjo katika uso wako. Wala hauhitaji kutumia bidhaa za kemikali kwa kula tu vyakula vya asili utaondokana na hali hiyo.

Matunda yenye majimaji na mboga za majani huleta unyevunyevu na kukufanya uonekane na ngozi ya ujana. Katika lishe yako ongeza tikitimaji, nyanya, tango na limau.

Vile vile kula kabichi kwani lina vitamini C na vitamini A, ambazo zote zinasaidia kuondoa mistari.

Pia hutoa sumu katika damu na nyuzi nyuzi katika kabichi zinasukuma taka na sumu kutoka mwilini. Sumu zinaweza kuonekana usoni na kukufanya uonekane mzee kuliko umri wako

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi