loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Askofu Gamanywa amesema kweli

J UZI gazeti hili liliripoti kuhusu uzinduzi wa kitabu cha ‘Uzalendo na Falsafa ya Mamlaka’ kilichoandikwa na Mwangalizi Mkuu wa WAPO MISSION INTERNATIONAL, Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa aliposema haiwezekani kumtenganisha Rais John Magufuli na maslahi ya Taifa.

Kwamba hii inatokana na uwezo mkubwa alio nao na aliuonesha Rais Magufuli katika kusimamia na kudhibiti usalama wa maslahi ya Taifa bila kujali maslahi ya vikundi vya kisiasa, kidini na kimaeneo.

Sisi tunampongeza Askofu Gamanywa kwa kusema ukweli kuwataka Watanzania kuwa makini ili wasikengeuke kwenda kupiga kura za usaliti katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 wa rais, wabunge na madiwani, badala ya kupiga kura za uzalendo.

Sisi tunasema hivyo tukijua wazi kuwa, kuwapo kwa maslahi ya taifa, ni suala moja na kuwapo kwa mtu mwenye uwezo wa kusimamia, kudhibiti na kulinda maslahi ya taifa kama ilivyo kwa Rais Magufuli ni suala lingine.

Tunaungana na Askofu Gamanywa na wote wenye mapenzi mema kwa Tanzania kusema licha ya kuwapo wagombea wa vyamambalimbali wanaojinadi ili wachaguliwe kushika mamlaka ya nchi, kila Mtanzania hasa mzalendo wa kweli, lazima atapiga kura ya uzalendo kwa kumchagua kiongozi mwenye sifa na uwezo na uzoefu wa vitendo kutetea, kusimamia na kulinda maslahi ya Tanzania.

Tunaungana na kiongozi huyo wa dini kuwasisitiza Watanzania kutathmini ilani za vyama kwa kigezo cha maslahi ya taifa yasiyohusisha viashiria vya kumoboa misingi ya utaifa wa Watanzania na kuwarudisha kwenye maslahi ya vikundi na maeneo ya kikanda.

Kimsingi, chama au sera ya chama inayozungumzia maslahi ya makundi, badala ya maslahi ya taifa, ni hatari kwani inalenga kuwarudisha Watanzania katika viwango vya ubaguzi wa kimaeneo na kimakundi walivyokwishavivuka.

Tunapompongeza Askofu Gamanywa kwa kuwa mkweli na jasiri kusema waziwazi kuwa Watanzania wazipuuze ilani za wagombea na vyama vinavyopinga mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa na badala yake, vinajikita katika nadharia za maslahi na itikadi za vikundi.

Sisi tunasema, tunaukubali ukweli aliousema Gamanywa kuwa sasa zipo dalili za kuwapo ushindani wa kisiasa usio wa ushawishi wala unaojikita katika ubora wa ilani zinzosimamia na kulinda maslahi ya taifa, bali unaojikita katika maneno ya chuki, shutuma, tuhuma, na hisia zilizojaa hasira na vinyongo.

Tunasema, kuchagua wagombea na vyama yenye ilani za namna hiyo, ndiko kupiga kura kura za usaliti dhidi ya Tanzania na watu wake.

JUZI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi