loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KMC, Namungo kila mmoja ana lake

MZUNGUKO wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaendelea leo kwa baadhi ya timu kucheza viwanja mbalimbali, ambapo KMC itakuwa mwenyeji wa Coastal Union na Namungo dhidi ya Kagera Sugar.

KMC iliyoanza kwa kasi michuano hiyo na baadaye  kushuka taratibu huenda wakatumia mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Uhuru kumaliza hasira zao baada ya kutoka kupoteza michezo miwili iliyopita.

Ilipoteza dhidi ya Polisi Tanzania na Kagera Sugar kila mchezo kwa bao 1-0, matokeo yaliyowashusha kutoka nafasi za juu hadi nafasi ya saba.

Wanakutana na Coastal Union ambao pia hawana matokeo mazuri kwani katika michezo mitano wameshinda mmoja na sare moja, mingine wakipoteza.

Coastal nayo pia imetoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga waliofungwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo ziliwahi kukutana msimu uliopita kwenye uwanja huo wa Uhuru na Coastal haitasahau kipigo cha mabao 5-2, hivyo utakuwa ni mchezo mgumu kwa kila mmoja wote wakitoka kujeruhiwa.

Namungo iliyoanza na mwenendo mbaya itakutana na Kagera katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi. Timu zote mbili zimetoka kupoteza michezo iliyopita dhidi ya Mwadui bao 1-0 na dhidi ya Azam FC mabao 4-2.

Pia Biashara United itachuana na Ihefu katika Uwanja wa Karume, Mara. Timu hiyo imekuwa ikijitahidi kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kupata matokeo.

Katika michezo mitano imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja ikiwa na pointi 10, huku Ihefu ikiwa iko nafasi ya pili kutoka mwisho na pointi tatu ilizovuna katika mchezo mmoja na mingine minne ikitoka kupoteza.

JKT Tanzania itachuana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, wote wawili wakitoka kupoteza michezo yao iliyopita.

Wenyeji wametoka kufungwa na Simba mabao 4-0 na bado haiko vizuri ikishinda mchezo mmoja tu kati ya mitano, ikipata sare moja na kupoteza mitatu na Ruvu pia wameshinda mmoja, sare mbili na kupoteza miwili.

Timu hizo kila moja ina udhaifu wakw, Ruvu safu yake ya ushambuliaji imefunga bao moja na kwenye ulinzi wamefungwa mabao matatu lakini bado wako vizuri kuliko JKT iliyofungwa mabao nane na kufunga mawili.

Mchezo huo ni mgumu na muhimu kwa kila mmoja kushinda na mbinu za makocha wao ndizo zitakazowapa ushindi.

NYOTA mkongwe wa muziki ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi