loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaoishi mabondeni chukueni tahadhari

MVUA zilizoanza kunyesha Jiji Dar es Salaam tangu juzi na sehemu nyingine nchini ni kuashiria kuanza kwa kipindi cha mvua za vuli. Madhara ya mvua hizo yameanza kuonekana baada ya kutokea vifo wa watu sita kwa siku ya kwanza juzi Jumanne wiki hii.

Mbali na vifo vilivyosababishwa na mvua hiyo, pia madhara mengine yaliyosababishwa na mvua hizo ni kufungwa kwa barabara kadhaa za Jiji la Dar es Salaam, maji kuingia ndani na vifaa vya ndani kuelea.

Eneo korofi zaidi ni jangwani. Kutokana na kujengwa majengo eneo la jangwani ambalo ni mkondo wa maji kumesababisha kutuama maji na kuleta adha kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Madhara yanaweza kuongezeka zaidi kutokana na taarifa ya hali ya hewa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambapo ilitangaza kuwa mvua kubwa zaidi inatarajia kunyesha, ikiwa ni mwendelezo wa ile iliyoanza kunyesha maeneo ya visiwani Unguja na Pemba, Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, ikiwa ni kuziba kwa mitaro inayopitisha maji, maeneo mengi ya Dar es Salaam kutokuwa na mitaro imara ya kuhimili kupitisha maji mengi kwa wakati mmoja, pia kubwa zaidi ni wananchi kuendelea kujenga na kuishi mabondeni maeneo ambayo serikali imekwishapiga marufuku kwa ajili ya usalama.

Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka ya Hali yaHewa imetangaza pia vipindi vya upepo mkali unaofikia km 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Shime wakazi wa mabondeni, mfuate ushauri wa mamlaka husika za hali ya hewa na serikali ili kuweza kuokoa maisha ya watu, kuepusha madhara makubwa ambayo hutokea kila mara inyeshapo mvua kubwa

VYAMA vingi vya michezo ...

foto
Mwandishi: Dativa Minja

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi