loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ni mpambano wa Guardiola, Arteta

MANCHESTER City itakuwa ikisaka ushindi wake wa pili wa Ligi Kuu ya England tangu kuanza kwa kampeni zake msimu huu wakati itakapoikaribisha Arsenal leo, Hatahivyo, wenyeji Man City katika mchezo huo wa Etihad, watatakiwa kuwa makini na ingizo jipya la Arsenal, Thomas Partey ambaye anatarajia kuwa uwanjani leo.

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kiliisambaratisha the Gunners katika mchezo wa kwanza ulipoanza msimu wa mwaka 2019/20 wa Ligi Kuu, wakishinda 3-0 kwenye Uwanja wa Etihad Juni.

Lakini Arteta alifanikiwa kulipa kisasi dhidi ya mwajiri wake huyo wa zamani, pale kikosi chake kiliposhinda 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Wembley katika nusu Fainali ya Kombe la FA.

Arteta amekiimarisha kikosi cha Arsenal tangu alipowasili katika klabu hiyo Desemba 2019 na amekiongezea nguvu kwa kusajili katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Kocha huyo alimsajili Gabriel Magalhaes, ambaye alikuwa chaguo lake namba moja pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Ghana, Thomas Partey kutoka Atletico Madrid.

Partey alikuwa ka- tika rada za the Gunners kwa takribani miezi 12 na mchezaji huyo alikuwa akilitumikia taifa lake wakati wa mapumziko ya ligi kupisha mechi za kimataifa, ataichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo dhidi ya City. Guardiola amekuwa akiwatumia viungo wazuiaji wawili, ambao ni Fernandinho na odri katika mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu za msimu huku akitarajia kumtumia Partey ambaye anatawala sehemu ya kiungo.

Arteta anatarajia kumuanzisha Granit Xhaka kama kiungo pekee wa kati, huku Partey na Dani Ceballos wakiwa mbele ya mchezaji huyo.

Mfumo huo utamsaidia mchezaji huyo mpya wa Arsenal kukimbia katika safu ya ulinzi ya Man City na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji waliokuwa mbele yake, lakini mabeki watakuwa mbele yake kuzuia nafasi asilete madhara.

MSHAMBULIAJI wa AC Milan, ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi