loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yarejesha kwa wakulima Bil 1.3/-

TAASISI YA kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Tabora imefanikisha kurejesha kiasi cha Sh 1,348,675,330.87 kwenye vyama vya msingi AMCOS na wananchi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita

Akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Tabora Musa Chaulo alisema kwamba kwa kipindi cha mwezi wa Julai hadi Septemba mwaka huu walifanikisha kurejesha kiasi kikubwa cha fedha .

Alisema kiasi cha Sh 1,163,717,560.80 ni za wakulima wa tumbaku waliokuwa wameuza lakini hawajalipwa muda mrefu kutoka kampuni ya Magefa Growers Limited kwa vyama vya msingi AMCOS 12 katika wilaya ya Urambo.

Chaulo alisema kwamba vyama vingine ni AMCOS 11 katika wilaya ya Kaliua fedha hizo zilikuwa ni za msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2019/2020.

Aidha Kamanda huyo wa Takukuru mkoa wa Tabora aliendelea kusema kwamba Sh 103,446,770.07.

zilirejeshwa kwa wakulima wa tumbaku wa Chama cha Msingi Ushirika Imalamakoye AMCOS katika wilaya ya Urambo baada ya kubaini kuna wakulima waliuza tumbaku kwenye soko la kwanza pasipo mkataba wa kulima tumbaku na kuwakosesha haki wakulima waliokuwa na mikataba ya kuuza kwenye soko la kwanza.

Chaulo alisema pia Takukuru iliweza kufanikisha kiasi cha Sh 16,500,000 kurejeshwa kwa Nyota Muungano AMCOS zikiwa ni fedha zilizookolewa kwenye malipo ya ujenzi wa ghala wakati halikujengwa.

Alisema pia kuwa Sh 220,000 zilirejeshwa kwenye chama cha Ushirika cha Nsenda AMCOS wilayani Urambo, mkoani hapa na kuongeza kuwa kiasi cha Sh 25,443,000 kilirejeshwa na chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku WETCU baada ya kukatwa kimakosa kama gharama ya kusambaza mifuko 660 ya mbolea ya NPK kwa MTAZAMO AMCOS Ya Kaliua msimu wa kilimo 2013/2014.

Kamanda huyo wa Takukuru alisema kwamba fedha kiasi cha Sh milioni 1.2 kilireshwa kwa mwananchi Kadala Mwigulu wa kijiji cha Ntiliga Mdaka baada ya kuombwa rushwa ya Sh 1,700,000 ili asifikishwe polisi kwa madai alihusika kwenye mauaji ya mke wake.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi