loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yatoa tril 2/- mikopo ya wanafunzi

SERIKALI imetoa jumla ya Sh trilioni 2.25 katika miaka mitano iliyopita kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo aliyasema hayo juzi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na maofisa mikopo kutoka taasisi za elimu ya juu.

Dk Akwilapo alisema kutokana na dhamira ya serikali, bajeti ya fedha za mikopo imekuwa ikiongezeka hadi kufikia Sh bilioni 464 kwa mwaka wa masomo 2020/21 kutoka Sh bilioni 348.7 mwaka 2014/15.

“Kwa ujumla, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali imetoa jumla ya Sh trilioni 2.25 kiasi hiki cha fedha, kingeweza kutumika katika miradi au matumizi mengine, lakini serikali inatambua umuhimu wa kuwawezesha vijana wake kupata elimu ya juu na mchango wa elimu ya juu katika maendeleo ya nchi,” alisema.

Dk Akwilapo alisema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha wananchi hasa wanafunzi wahitaji wanapata mikopo kwa ajili masomo ya elimu ya juu ili watimize ndoto zao na washiriki shughuli za kijamii na kiuchumi za kuliendeleza taifa.

‘’Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015, jumla ya wanafunzi waliokuwa wanapata mkopo kwa mwaka ilikuwa wanafunzi 98,300 lakini mwaka jana (2019/20) walikua 132,392 na mwaka 2020/21 tumepanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 145,000.

“Wanafunzi hawa 145,000 watapata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 464, hivyo basi, tukisema serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya dhati ya kuwawezesha wanafunzi kutimiza ndoto zao, tunathibitisha kwa takwimu kama hizi,” alisema.

Dk Akwilapo alisema Rais Magufuli amekuwa akielekeza wanafunzi na vyuo walipwe kwa wakati na kwamba hilo linatekelezwa na aliagiza HESLB ihakikishe inakamilisha uchambuzi wa maombi ya mikopo, itoe orodha na kutuma fedha vyuoni mapema.

Aliagiza pia kuanzia robo ya pili ya mwaka huu wa fedha, bodi hiyo iongeze kasi ya utoaji wa elimu na kukutana na wadau ili kuwaelimisha kuhusu taratibu za urejeshaji mikopo na kuzitaka taasisi za elimu ya juu ziimarishe madawati wa mikopo katika maeneo yao ya kazi ili yatoe huduma inayotarajiwa na serikali kwa wanafunzi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB, Profesa William Anangisye alisema wataendelea kuhakikisha fedha ambazo serikali inazitoa kwa bodi ya mikopo zinatumika kama ilivyokusudiwa

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Bahi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi