loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waangalizi EAC wa Uchaguzi Mkuu kuwasili Oktoba 23

WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kufi ka nchini mwishoni mwa wiki ijayo tayari kwa uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Ujumbe huo utaongozwa na Rais mstaafu wa Burundi, Sylvestre Ntibantunganya na utapelekwa katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar. Taarifa ya EAC kwa vyombo vya habari jana kutokea makao makuu ya jumuiya hiyo, Arusha, lieleza kuwa itapeleka waangalizi wa uchaguzi mkuu nchini na watafika Oktoba 23.

Hatua hiyo inatokana na Mkataba wa Kuundwa kwa jumuiya hiyona mwaliko wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) na uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu uangalizi wa uchaguzi katika nchi za EAC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jukumu la ujumbe huo ni kuangalia mazingira ya uchaguzi, shughuli za kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi, kuhesabu kura na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, ujumbe huo utakuwa katika mikoa mbalimbali ya Bara na Zanzibar baada ya mkutano na waandishi wa habari wa ufunguzi rasmi wa jukumu hilo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 24, jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo unahusisha waangalizi kutoka maeneo mbalimbali wakiwamo wabunge wa bunge la EAC, mawaziri wanaohusika na masuala ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama, Tume za Kitaifa za Uchaguzi na vijana mabalozi wa EAC.

Watanzania hawatahusika katika ujumbe huo wa waangalizi kutokana na kanuni za uangalizi na tathimini zinazozuia raia wa nchi yenye uchaguzi kutohusika kufuatilia uchaguzi katika nchi yake mwenyewe.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Libérat Mfumukeko, alisema uangalizi huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Mkataba wa Kuanzishwa kwa jumuiya hiyo unaotaka kuheshimu misingi ya kimataifa ya utawala wa kidemokrasia sambamba na kanuni za uangalizi na tathimini za EAC.

Katibu Mkuu alibainisha kuwa “kadri jumuiya inavyozidi kuingia katika mchakato wa mtangamano na lengo kuu la kuwa na shirikisho la kisiasa, nchi wanachama wa EAC zinahitaji kuweka sawa shughuli zao za utawala na zinapaswa kuweka kipaumbele michakato ya kisiasa na uchaguzi wa kila mmoja wao”.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi