loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mama, watoto waliokufa moto kuagwa leo Dar

TAKRIBANI saa nzima ilitumika kujaribu kuokoa maisha ya watoto watatu, mama yao na shangazi waliofariki kwa ajali ya moto katika eneo la Pugu Stesheni, Dar es Salaam.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na leo wanaagwa kabla ya kusafirishwa kwenda Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa maziko.

Watu waliofariki dunia ni Jackline Frank na watoto wake watatu, Edwin Katem(8), Edson Katemi(6) na Ivon Katemi(4) pamoja na wifi yake, Esther Katemi. Imeelezwa kuwa pamoja na watu hao kutolewa nyumbani salama bilka kubabuliwa na moto walifariki dunia.

Ilielezwa kuwa mfumo wa ujenzi wa nyumba hiyo ikiwamo madirisha kuwekwa nondo kulisababisha juhudi za kuokoa kwenda polepole sana. Akisimulia mkasa huo, baba wa familia hiyo, Edward Katemi alisema kuwa kwa sasa amebaki na mtoto mmoja, Erick Katemi aliyekuwa amehamishiwa shule ya bweni na aliondoka nyumbani hapo siku moja kabla ya ajali hiyo.

Katemi alisema wakati moto unaanza kuunguza nyumba hiyo, ndiyo alikuwa amefika kwenye lango la nyumba yake hivyo alikuwa mtu wa kwanza kuuona ulivyokuwa ukianza kuunguza sehemu ya mbele ya sebule yake na kushika kasi.

Alisema alishuka kwenye gari na kuita majirani kuomba wamsaidie kuuzima huku wakijitaidi kuwaita watoto na mkewe ambao kwa muda huo hawakuwepo sebuleni bali walikuwa vyumbani

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa ajali hii ambayo imechukua maisha ya familia yangu ni pigo kubwa kupoteza watoto watatu, mke na mdogo wangu, nawaombea kwa Mungu,”alisema Katemi.

Kwa mujibu wa Peter Katemi ambaye ni mdogo wa baba huyo mwenye nyumba, jitihada za kuwaokoa wanafamilia hao ziliendelea kwa takribani saa nzima kabla ya kufanikiwa kuwatoa wakiwa katika hali mbaya baada ya kutoboa ukuta.

“Tulishindwa kubomoa madirisha kutokana na nondo zilizowekwa,” alisema. Peter alisema ingwa waokoaji walikuwa na hofu ya kuingia na kudhibiti moto huo kutokana na kuhofiwa kuwa ulitokana na hitilafu ya umeme, walitumia maji kumwagia sehemu ya sebule lengo likiwa ni kuingia ndani.

“Wakati wengine wakimwagia maji, wengine walizunguka upande wa nyuma ya nyumba hiyo kwenye chumba cha kulala watoto kisha wakavunja ili kupata tobo la kuingilia ndani,” alisema.

Alisema walivunja eneo kubwa na kuwezesha baadhi ya watu kuingia ndani na kisha wakaenda kufungua mlango mkubwa. Waliwakuta watoto wawili wakiwa kwenye chumba hicho kilichotobolewa huku mama yao akiwa chumbani kwake na mtoto mdogo, Ivon.

SHIRIKISHO la Vyama Vya Watu ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi