loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zitto arejea Kigoma kuendelea na kampeni

POLISI mkoani Kigoma wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo nje ya Kiwanja cha Ndege cha mjini hapa waliopofi ka kumpokea mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kabwe Zitto kwa kuzuia shughuli nyingine za kijamii kuendelea.

Upigaji mabomu huo ulitokea wakati Zitto akiwa bado hajawasili mkoani Kigoma ambalo aliwasili ya saa tatu asubuhi, akitokea jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege nchini (ATCL) ambapo alikuwa akipata matibabu,baada ya kupata ajali Oktoba 6, Mwaka huu, akiwa katika ziara ya kufanya mikutano ya kampeni jimbo la Kigoma Kusini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama, akizungumza mjini Kigoma alisema kuwa jeshi lake halikujihusisha kwa namna yeyote na ziara ya kiongozi hiyo na kwamba kama hiyo imetokea inawezekana watendaji wa jeshi hilo walikuwa wakitimiza majukumu yao katika kusimamia amani na usalana.

Sambamba na hilo Kamanda Manyama alikanusha taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao walikuwa kwenye msafara wa kiongozi huyo akisema taarifa hizo ni za uzushi.

Baadhi ya wafuasi wa chama hicho wamelalamikia vitendo vya upigaji mabomu na kukamatwa kwa baadhi ya wafuasi hao.

Saimon Alexander, mkazi wa Ujiji, Mjini Kigoma alisema kuwa walikuwa wakimuombea dua kiongozi wao ili aweze kupona na kurudi katika majukumu yake ya kila siku, lakini wameshangazwa na kitendo cha jeshi hilo kuwapiga mabomu ingawa waliendelea na suala la kumpokea mgombea wao.

Akizungumza na wananchi katika ofisi za mkoa za chama hicho Ujiji Mjini Zitto aliwashukuru wananchi hao kwa upendo waliouonesha kwenda kumpokea.

“Nashukuru Mungu nimerudi salama nikiwa na afya njema tutazungumza zaidi kwenye mikutano na nipo hapa kuhakikisha tunapigania jimbo letu hadi kieleweke,” alisema

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi