loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM atumia mtandao wa kijamii kuomba kura

IKIWA zimebakia siku 11 kabla ya kuhitimisha kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ameamua kutumia mtandao wa kijamii kuomba kura kwa Watanzania.

Magufuli ambaye anaendelea na kampeni baada ya kutembelea mikoa mbalimbali nchini, katika ukurasa wake wa twitter ameanza kwa kujitambulisha jina lake na chama chake na kisha kuwaomba wananchi wamchague.

“Naitwa John Pombe Joseph Magufuli, mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ewe Mtanzania mwenzangu, naomba kura yako ya ndio tarehe, 28/10/2020. Chagua Magufuli kwa maendeleo ya kweli ili tuendelee kujenga Tanzania mpya. Asante,” ulisema ujumbe huo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM, Ally Bashiru, baada ya kuhitimisha kampeni jijini Dar es Salaam, sasa Magufuli anaanza awamu nyingine ya kampeni katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na kisha ataingia Dodoma.

Bashiru alisema mpaka juzi, CCM kimefika maeneo yote nchini. Alisema kutokana na ufinyu wa muda, Rais Magufuli hatakwenda katika baadhi ya mikoa ambayo hata hivyo mgombea mweza, Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa wamefika.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi