loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bashiru: Mitandao haipigi kura

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally ameeleza kuwa kutokana na kazi kubwa iliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano anawahakikishia wanaCCM kuwa chama hicho kitashinda majimbo yote ya mijini na kutetea waliyonayo tayari likiwemo jimbo la Nyamagana kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

Dk Bashiru amebanisha hayo alipokuwa katika mkutano wa hadhara jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, katika Viwanja vya CCM Kirumba leo.

“Nyamagana kwa majimbo yaliyopo mijini, ndio moja ya majimbo ambayo tuna uhakika wa kushinda, lakini niongeze zaidi tuna uhakika wa kushinda majimbo yote ya mijini mwaka huu,” amesema.

Dk Bashiru ameeleza kuwa baada ya wapinzani kuona CCM ina uhakika wa kushinda majimbo mengi zaidi kuliko ya mwaka 2015, wameanza kuhamasisha fujo siku ya kupiga kura na wameanza mapema katika baadhi ya miji ikiwemo Pemba, Chemba, Njombe na maeneo mengine na kwa visingizio vya kuibiwa kura.

“Ndio maana mnasikia zile ngonjera za tutaingia barabarani, tunataka kuibiwa kura, wanaingia kwenye mitandao isiyokuwa na wapiga kura, wanatafuta umati wa watu wakimbizi wanaunganisha na umati wa watu wanaokwenda kuzimamoto wanasema nyomi hiyo. Mitandao haipigi kura mitandao haijajiandikisha wanaopiga kura ni Watanzania wenye sifa na walioandikishwa, waache kufanya siasa za kuomba kura kwenye mitandao waende nyumba kwa nyumba kama wanaweza,” amesema.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amezipongeza jumuiya zote za chama hicho pamoja na kamati za ushindi kwa kuendelea kukitafutia kura chama hicho tangu kuanza kwa kampeni mpaka sasa zinapoeleka ukingoni.

Pia Dk Bashiru ameeleza baadhi ya sababu zinazokifanya chama hiko kuendelea kuwa imara kuliko wakati mwingine wowote kuwa ni pamoja na nidhamu ya chama hicho, moyo wa kujitolea kwa wanachama wote hasa katika kipindi hiki cha kutafuta ushindi wa chama, pamoja na kuwa na ilani bora kuliko vyama vingine vyote inavyoshindana navyo.

Wakati huo huo, Mgombea ubunge wa jimbo la Nyamagana Stansilaus Mabula ameushukuru  uongozi wa chama hicho wilaya ya Nyamagana na wanachama wote kwa kuendelea kuwa na mshikamano, umoja, na moyo wa kujitolea tangu kuanza kwa kampeni mpaka sasa na alimhakikishia Katibu Mkuu ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 28, mwaka huu.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Dk Anthony Diallo.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi