loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbatia siku 7 kusugua benchi

KAMATI ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi jimbo la Vunjo limemfungia kwa siku saba Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia amefungiwa siku saba kufanya kampeni zake.

Kamati hiyo ya maadili imemfungia Mbatia kwa kile ilichoeleza kuwa ni kutumia kutumia kipeperushi ambacho hakijaidhinishwa na msimamizi wa uchaguzi na adhabu hiyo itaisha Oktoba 23.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi amethibitisha kusimamishwa kuendelea lakini amepinga kufungiwa kwa kile alochodai kuwa ni batili.

 “Ni kweli wamenisimamisha lakini nimeshangaa maana walipotaka nipeleke utetezi kuhusu hicho kipeperushi tuliwapelekea na ushahidi wa barua iliyokitambulisha hicho kipeperushi,” amesema Mbatia.

Aidha kikao hicho cha kamati ya maadili Vunjo kilichokaa jana Oktoba 16 kilikaa na kupitia  tuhuma za uvunjifu wa maadili ya uchaguzi na kumkuta na hatia ya kukiuka maadili hayo.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi