loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk. Bashiru: Tutatumia kila mbinu kushinda Ilemela

 

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi nchini,Dk Bashiru Ally amesema chama chao kitatumia kila mbinu kuhakikisha kinashinda katika uchaguzi mkuu haswa katika nafasi ya ubunge kwenye jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.

Dk Bashiru alisema hayo wakati wa mkutano na mabalozi wa chama hicho katika uwanja wa CCM Kirumba. Dk Bashiru alisema watatumia kila mbinu ili mgombea wa Chama chao nafasi ya ubunge Ilemela anashinda.

‘’ Tutatumia kila mbinu kushinda Ilemela,na huo ujumbe ufike kwa yoyote anaeota ndoto, CCM kupoteza Ilemela haiwezekani.Dk Mabula ameteuliwa kutokana na sifa ya uchapakazi na amefanya makubwa kitaifa na mawaziri shupavu ambao kwa namna yoyote tunapambana mpaka arudi tena bungeni’’alisema Dk Bashiru.

Dk Bashiru alisema  Dk Mabula ni mmoja ya wakina mama 24 katika wagombea wanawake nchi nzima waliochaguliwa na chama chao. Alisema chama chao kimedhamiria kuhakikisha wagombea wote wanawake wanashinda.

‘’Kama ingekuwa matambiko tungesema Ilemela ndio matambiko makuu ya ushindi.Ilemela ni moja ya majimbo kati ya majimbo 24 tulioweka mkakati malumu wa ushindi’’ alisema Dr Bashiru.

Kwa upande wake mgombe wa ubunge jimbo la Ilemela kupitia CCM,Dk Angelina Mabula alisema ataendelea kushirikiana vyema na wakazi wa Ilemela na kuhakikisha anawaletea maendeleo.

Alisema tokea azindue kampeni zake amekuwa akiwaeleza wananchi maendeleo rais John Magufuli aliofanya kitaifa na kwa wilaya ya Ilemela.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi