loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man Utd yamuongezea amuongezea mkataba Pogba

KLABU ya Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo, Paul Pogba hivyo ataendelea kusalia Old Trafford hadi Juni 2022. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, raia wa Ufaransa angekuwa amemaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.

Pogba ameanza mechi tatu za Ligi Kuu za United msimu huu, ikiwa ni pamoja na ule waliopigwa nyumbani kwa 6-1 na Tottenham.

Kipindi cha mapumziko ya kimataifa, Pogba alisema anahamia kwa miamba ya La Liga, Real Madrid itakuwa ndoto.

Inaeleweka uamuzi wa kuongeza mkataba wake ulichukuliwa wiki chache zilizopita, kabla ya maoni ya Pogba.

Pogba alijiunga tena na United akitokea Juventus kwa rekodi ya klabu paundi milioni 89 mwaka 2016. Jeraha la kifundo cha mguu lilimzuia kucheza michezo 22 msimu uliopita.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi