loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbappe aipaisha PSG

Kylian Mbappe juzi alifunga mabao mawili na timu yake ya Paris St-Germain (PSG) walipocheza na Nimes iliyokuwa na wachezaji 10 kwa dakika 78 na kushinda kwa mabao 4-0.

Mbappe alimzunguka kipa na kupachika wavuni bao katika kipindi cha kwanza kabla ya kukimbia ili kufunga bao lake la pili na kuifanya PSG kuwa na mabao 3-0. Beki wa pembeni Alessandro Florenzi alifunga kwa kichwa cha karibu baada ya kugonga nguzo mara mbili.

Na Mhispania Pablo Sarabia, ambaye alianzishiwa na Florenzi, alifunga bao la nne na kuifanya PSG kushinda 4-0. Beki wa Nimes Loick Landre alitolewa nje kwa mchezo usio wa kiungwana baada ya kumshika tumboni Rafinha dakika ya 12.

Kiungo Rafinha,ambaye alijiunga na mabingwa wa Ufaransa kwa makubaliano ya miaka mitatu kutoka Barcelona mwezi huu, alikuwa mzuri wakati wote na alikuwa msaada kabla ya kubadilishwa katika kipindi cha pili.

PSG walimkosa mshambuliaji wao muhimu Neymar, ambaye alikuwa nje baada ya kuichezea Brazil na kufunga hat-trick katika ushindi wao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Peru Jumatano iliyopita.

Mshambuliaji wa Everton Moise Kean, aliyejiunga na PSG kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, alicheza kwa mara ya kwanza lakini hakuweza kufunga bao lakini vichwa vyake viligonga mwamba mwishoni mwa kipindi cha pili.

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi