loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ronaldo amevunja sheria za afya-Waziri

WAZIRI wa michezo Italia, Vincenzo Spadafora amesema Cristiano Ronaldo huenda akawa amevunja sheria za afya wakati aliporejea Italia mara baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona alipokuwa Ureno.

Mshambuliaji huyo wa Juventus alirejea Italia na ndege binafsi Jumatano iliyopita na kujiweka karantini nyumbani kwake. Spadafora aliulizwa katika mahojiano na kipindi cha radio ikiwa Ronaldo amevunja sheria za afya kwa kufanya hivyo, akajibu: ”Ndiyo nadhani hivyo, kama hakukuwa na idhini maalumu kutoka katika mamlaka ya afya”.

Hata hivyo, rais wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli amemkingia kifua mchezaji wake kwa kusema hakuna sheria iliyovunjwa. “Lazima upige simu kwa Waziri wa Afya na Waziri wa Mambo ya Ndani waeleze kitu gani kimekiukwa,” alisema Agnelli.

Jumatano Juventus ilisema Ronaldo amerejea kwa ndege ya matibabu iliyoidhinishwa na maofisa wa afya.

Ronaldo alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania na wa UEFA Nations League akiwakabili Ufaransa na kushindwa kucheza dhidi ya Sweden kutokana na kukutwa na virusi vya corona wakati Ureno ikichomoka na ushindi wa mabao 3–0 katika mechi hiyo Jumatano iliyopita.

foto
Mwandishi: ROME, Italia

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi