loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

LIVERPOOL, CHELSEA ZABANWA

TIMU za Liverpool na Chelsea jana zilibanwa mbavu baada ya kulazimishwa sare katika michezo ya Ligi Kuu. Liverpool ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Everton kwenye dimba la Goodison Park na kuifanya Everton kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Sare hiyo katika mchezo huo unaifanya Everton kufikisha pointi 12 katika michezo mitano iliyocheza mpaka sasa na Liverpool, ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wanashika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 10.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Saidio Mane lakini walipata pigo dakika ya 15 baada ya kwa beki Vigil van Djik kuumia na kulazimika kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Gomez.

Everton walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 19 kupitia kwa beki Michael Keane na timu hizo kulazimika kwenda mapumziko kwa kufungana bao 1-1. Dakika ya 72 Mohamedi Salah alifunga bao la pili lakini Everton walisawazisha bao hilo dakika ya 81 kupitia kwa Dominic Calvert-Lewin.

Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson alifunga bao dakika ya 90+2 lakini teknolojia ya VAR ililikataa bao hilo kwa kigezo mshambuliaji Sadio Mane aliyekuwa kwenye eneo la kuotea aliingilia shambulizi.

Chelsea ikicheza nyumbani ilitoka sare ya mabao 3-3 na Southampton ambapo Annik Vestergaard alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi na kuifanya Southampton kugawana pointi na Chelsea

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi