loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi kuwa na sauti kwenye uendeshaji wa uchumi

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema kuwa Serikali imejipanga kujenga uchumi wa kitaifa, kwa kuwapa uhuru wananchi kuwa na kauli ya namna ya kuendesha uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.

Makamu wa rais huyo amesema hayo muda mfupi uliopita alipomwakilisha Rais John Magufuli, kwenye mkutano wa sekta binafsi uliolenga kumpongeza Rais Magufuli kwa mafanikio ya miaka mitano ya uongozi wake.

Amesema kuwa sekta binafsi ina mchango mkubwa kwenye  kujenga uchumi wa Tanzania, kwakuwa ndiyo wadau wakubwa katika kuielekeza Serikali namna bora ya kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini. 

“Tutahakikisha tunaendelea kulinda haki za wafanyabiashara kwenye uendeshaji wa biashara zao na shughuli zozote za kiuchumi zinazofanyika hapa nchini” amesema Samia Suluhu.

Katika hatua nyingine makamu wa rais aliahidi pindi mchakato wa uchaguzi utakapokamilika, kitaitishwa kikao cha wafanyabiashara wote nchini kitakachokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali  yatakayokuza sekta ya biashara.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi